Balotelli akaribishwa Juventus - Pirlo amwita

Andrea Pirlo ROME, ItaliaANDREA Pirlo ameshauri klabu yake ya Juventus kuvunja benki yao ya fedha na kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, Mario Balotelli.Pia ameitoa shaka klabu yake kutokana na tabia za utukutu za Balotelli, na kusema yeye anaweza kupewa jukumu la kumdhibiti.
Wachezaji hao wawili walikuwa kwenye kikosi cha Italia kilichoshiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya na kufika hatua ya fainali.
Kocha wa City, Roberto Mancini ana matumani Balotelli (21) atabaki dimba la Etihad msimu huu.
"Balotelli aje Juventus?, nadhani ni sawa ningependa aje," alisema Pirlo wakati akiongea na Sky Sport Italia.
Baada ya kuelezwa habari ujauzito za rafiki yake wa zamani wa kike, Raffaella Fico huenda Balotelli akashawishika kurejea Italia.
Akikaririwa na tovuti ya michezo ya Sport Mediaset, rafiki huyo wa kike alisema, Balotelli amefurahishwa na habari za kutarajiwa kuwa baba wa mtoto kwa mara ya kwanza.
Alisema: "Nilimpigia simu kabla ya mchezo dhidi ya Ujerumani, nikamweleza nina mimba, ni mtoto wako.
"Baada ya kukaa kimya, alinijibu kwa kuniambia nimempa habari nzuri kuwahi kuzipata."
Pirlo anaamini anaweza kumdhibiti mchezaji huyo mtata kama alivyofanya wakati wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya iliyofanyika Poland na Ukraine.
"Nafahamu jinsi ya kuongea naye," alisema na kuongeza: "Wote tunatoka Brescia na tunapokuwa kwenye kikosi cha taifa tunaongea vizuri.
"Haipo shida kumdhibiti, naweza kufanya kazi hiyo kwenye vyumba vya kubadilisha nguo. Ukweli alionyesha tabia nzuri.
"Nitafurahi aje Turin. Mario ni aina ya mtu unayehitaji kuwa naye karibu."
Juventus imepania kufanya usajili wa wachezaji wenye majina makubwa msimu huu kwa lengo la kujipanga kutetea taji lao na kuongeza nguvu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Lakini wanafahamu kwamba, mabingwa wa England--Man City hawako tayari kumuuza Balotelli

Post a Comment

Previous Post Next Post