Shirika la Save the Children, limeonya kuwa ukosefu
wa mvua ya kutosha na kuendelea kwa mzozo nchini Somalia, kunatishia
kusambaratisha mafanikio yaliyoafikiwa tangu mwaka uliopita, wakati
taifa hilo ilipokumbwa na baa la njaa.
Shirika hilo limesema ikiwa hali hiyo itaendelea, maisha ya maelfu ya watoto imo hatarini.
Shirika hilo la save the children, limesema
idadi kubwa ya familia nchini Somalia, hawana uwezo wa kukabiliana na
athari za ukame na kutoa wito wa kuongezwa kwa misaada zaidi ya dharura
nchini Somalia.
Wakati huo huo, shirika hilo limetoa wito wa
kubuniwa wa mikakati mipya ili kutambua na kusaidia taifa hilo
kukabialana na athari za baa la njaa.
Mashirika kadhaa ya kutoa misaada ya kibinadam
pia yametoa wito wa kuongezwa kwa misaada zaidi nchini Somalia, ambako
maelfu ya watu waliangamia kutokana na baa la Njaa mwaka uliopita.
Source:- BBC Swahili
Post a Comment