Milovan alisema juzi kuwa umahiri aliotumia kufunga bao hilo la kusawazisha kwa timu yake, limemfanya atamani kumpanga
dakika zote 90.
Kauli hiyo imekuja huku Simba ikikabiliwa na mechi ya robo fainali
dhidi ya Azam FC hapo kesho kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
Salaam.
Milovan alikwenda mbali zaidi akilifananisha na mabao adimu
yaliyofungwa kwenye michauno ya Euro 2012; katika fainali hizo, ambazo
Hispania chini ya Kocha wake Vicente Del Bosque ilitwaa ubingwa kwa
kuifunga Italia.
Milovan alisema licha ya Boban kutokuwa fiti, hivyo kusita kumwanzisha, anatamani kufanya hivyo katika mechi ya kesho.
“Boban ni mchezaji mzuri sana, ni mwenye umuhimu mkubwa katika timu,
kinachofanya nisimwanzishe ni kutokana na kuwa fiti,” alisema Milovan.
Hata hivyo, Milovan alisisitiza wachezaji wake hawajaelewana kutokana na wachezaji wake wengi kutozoeana.
Alisema pamoja na changamoto hiyo, bado vijana wake watapambana kusaka
ubingwa wa michuano hiyo huku akitoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa
wingi kutoa sapoti.
Simba imeshinda mechi moja tu dhidi ya Ports ya Djibout na kufungwa mabao 2-0 na URA kisha kutoka sare ya bao 1-1
إرسال تعليق