![]() |
| Kombe la Dunia 1966 England |
Mcheza soka maarufu wa Ureno
mwenye asili ya Msumbiji, aliyeichezea Timu ya Taifa ya Ureno na klabu
ya Benfica, Eusebio,ameagwa kutoka hospitali alikolazwa wakati wa kombe
la Euro 2012 nchini Poland.
Mchezaji huyo mkongwe aliyepewa jina la Black Panther akiwa ni balozi wa Ureno wa soka amekuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu. Eusebio anakumbukwa mno kwa mchango wake wa mabao yaliyoiwezesha Ureno kumaliza ya tatu kwenye Kombe la Dunia la mwaka 1966 nchini England.
Chanzo:- BBC SWAHILI

Post a Comment