Makamanda wakutana Dar kujadili hali ya usalama

Kongamano la kujadili hali ya usalama katika nchi za Afrika limefunguliwa jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na makamanda mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika.

Kongamano hilo lililowakutanisha makamada mbalimbali kutoka barani Afrika na Marekani, lililenga kutoa mafunzo ya kiusalama ndani ya nchi, mafunzo ya kijeshi, jinsi ya kutatua matatizo ndani ya nchi, pamoja na kujadili hali ya usalama
ya Somalia.

Mkuu wa majeshi ya Marekani barani Afrika, Jenerali Carter Ham, alisema kongamano hilo ni muhimu kwa makamanda wa vikosi mabalimbali ili kubadilishana mawazo na ujuzi katika ulinzi.

Naye Meja Jenerali Leonard Mndame, kutoka Tanzania alisema suala la ulinzi ni la umuhimu kwa kila nchi na kwamba mambo kama kutokuwepo kwa ajira, uchunmi mbovu pamoja na siasa ndivyo chanzo kikubwa cha machafuko katika nchi yoyote.

Kongamano hilo litakalokuwepo kwa muda wa siku mbili, limewajumuisha maofisa na makamanda mbalimbali kutoka nchi za Mali, Ghana, Zambia, Afrika Kusini na Marekani.
SOURCE: NIPASHE

Post a Comment

Previous Post Next Post