Ferguson 'amfuata' Van Persie

Family matters: RVP could join champions City ALEX Ferguson yuko mjini London na huenda akatumia fursa hiyo kumshawishi mshambuliaji 'aliyeikataa' Arsenal, Robin van Persie kwenda Manchester United.
Bosi huyo wa United anatarajia kuwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye sherehe ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Labour Party Sports kwenye Uwanja wa  Emirates.
Habari za ndani, zinadai kuwa Fergie bado ana ndoto ya kumshawishi Van Persie kwenda United hasa baada ya Madachi huyo kukataa kusaini mkataba mpya Arsenal.
United itashindana na hasimu wake mkubwa kwenye Jiji la Manchester, klabu ya Man City ambayo kwa muda mrefu imetajwa kumtaka nyota huyo.
Man City inajiandaa kumpunguza mzigo wa washambuliaji wake kwa kumruhusu Emmanuel Adebayor kusaini mkataba wa kudumu Spurs anakocheza kwa mkopo kwa sasa.
Van Persie, anaonekana kufaa kucheza mfumo wa kocha wa City, Roberto Mancini ambao unatoa fursa kwa washambuliaji kuzunguka.
Kocha Fergie angependa kuona Van Persie akicheza sambamba na Wayne Rooney kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Van Persie anataka suala lake Arsenal kumalizwa kabla ya klabu hiyo kuanza ziara ya maandalizi ya Ligi Kuu barani Asia, Julai 24 mwaka huu.
United inaondoka Jumatatu ijayo kwenda Afrika Kusini kwa ziara kama hiyo na kisha pia kusimama Shanghai, China.
Wakati huohuo, Kocha Arsene Wenger amewaambia maofisa wa Arsenal kuharakisha kumalizika suala la  Robin van Persie hata kama uamuzi ni kumuuza.
Wenger anatarajia kukutana ana kwa ana na Van Persie siku chache zijazo kwa lengo la kumshawishi kubaki Emirates.
Lakini kama atashindwa kufikia naye makubaliano, basi anataka auzwe haraka

Post a Comment

أحدث أقدم