Akifungua Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo, kujadili bajeti ya Mwaka 2011/12 na 2012/13 jana, Membe alisema kilichojitokeza ni kasoro na taratibu za fedha zilikiukwa na hakuna dalili zozote za wizi.
“Mwezi wa tatu
kwa kipindi cha wiki moja ziliingia fedha nyingi sana katika wizara
yetu, ambazo zilizokuwa za safari za Rais tulivyoona hivyo tukazizuia
kutumika,” alisema Membe.
Membe alisema baada ya kamati aliyounda
kumaliza uchunguzi wa mwanzo, ameiagiza kumaliza kazi hiyo mapema
iwezekanavyo ili kubainisha kasoro zilizojitokeza.
“Kasoro hizo
tutakapozibaini tutatoa barua za karipio kali kwa wahusika, hivyo
wafanyakazi wa wizara yangu kuweni na amani kwani hakuna aliyehusika,”
alisema Membe.
Fedha zinazochunguzwa ni zile zilitolewa kati ya Machi Mosi na 8, mwaka huu kwa ajili ya safari za Rais kwenda Geneva nchini Uswis, Brazil, Adis Ababa na Arusha.
Fedha zinazochunguzwa ni zile zilitolewa kati ya Machi Mosi na 8, mwaka huu kwa ajili ya safari za Rais kwenda Geneva nchini Uswis, Brazil, Adis Ababa na Arusha.
Kauli ya Membe inakuja
kipindi ambacho kumekuwa na taarifa kwamba, fedha zilizotolewa kutoka
Hazina ni Sh3.5 bilioni, wakati zilizokuwa zimepangwa kwa safari hizo ni
Sh2 bilioni.Fedha hizo zinadaiwa kutolewa Hazina na maofisa waliokuwa
wakikaimu nafasi mbalimbali kwenye wizara hiyo kwa ajili ya safari za
Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumza na waandishi wa habari Juni 18,
mwaka huu, Waziri Membe alisema wakati tukio hilo likitokea, yeye na
naibu wake, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mhasibu Mkuu, walikuwa
safarini na kwamba nafasi zao zilikuwa zinakaimiwa.
Kuhusu Balozi
Waziri Membe alisema ili kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa, Balozi zilizopo kwenye nchi mbalimbali zitatumika kuwachunguza watu wanaoomba visa ya kuja nchini.
Kuhusu Balozi
Waziri Membe alisema ili kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa, Balozi zilizopo kwenye nchi mbalimbali zitatumika kuwachunguza watu wanaoomba visa ya kuja nchini.
“Sasa hatutasubiri kumkagua mtu anapofika
uwanja wa ndege na kitakachokuwa kikifanyika, ni Balozi zetu sasa
zitakuwa chujio la kuchuja wale wote wanaoomba visa ya kuingia nchini
kwetu,” alisema Waziri Membe.
Mapendekezo haya nitayapeleka Baraza la Mawaziri kwa lengo la kupitisha pendekezo hili ambalo litasaidia kupunguza wahalifu wanaoingia nchini kinyume na taratibu.
Mapendekezo haya nitayapeleka Baraza la Mawaziri kwa lengo la kupitisha pendekezo hili ambalo litasaidia kupunguza wahalifu wanaoingia nchini kinyume na taratibu.
Uwajibika kazini
Waziri Membe aliwataka wafanyakazi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa umakini na ushirikiano, ikiwamo kuwapa nafasi vijana kwenda balozi za nje kupata uzoefu zaidi.
Waziri Membe aliwataka wafanyakazi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa umakini na ushirikiano, ikiwamo kuwapa nafasi vijana kwenda balozi za nje kupata uzoefu zaidi.
“Zinapotokea nafasi za kwenda nje tusipendeleane,
vijana wanatakiwa kupewa kipaumbele ili waende wakapate mazoezi na sio
kwenda walewale,” alisema Membe.
Waziri Membe aliwataka wajumbe wa kikao hicho kupitia bajeti ya mwaka 2011/12, pale ambako kuwalikuwa na changamoto ili kuhakikisha hazijirudii mwaka huu wa fedha.
Waziri Membe aliwataka wajumbe wa kikao hicho kupitia bajeti ya mwaka 2011/12, pale ambako kuwalikuwa na changamoto ili kuhakikisha hazijirudii mwaka huu wa fedha.
Post a Comment