KIEV, UkraineKIUNGO wa Hispania, Andres Iniesta ametwaa tuzo ya
uchezaji bora wa Euro 2012, huku mwenzake Fernando Torres akitwaa tuzo
ya ufungaji bora iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Ulaya ( Uefa)
jana.
Kiungo huyo wa Hispania mwenye miaka 28, aliyechangia
ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Italia usiku wa Jumapili iliyopita,
alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo ya fainali na Kamati ya Ufundi
iliyoundwa na watu 11.
Nyota huyo wa Barcelona alishindwa kufunga bao na kutegeneza moja katika fainali hiyo, lakini amepata tuzo hiyo kutokana na mchango wake wa jumla ulivyowawezesha Hispania kutetea taji lao.
Nyota huyo wa Barcelona alishindwa kufunga bao na kutegeneza moja katika fainali hiyo, lakini amepata tuzo hiyo kutokana na mchango wake wa jumla ulivyowawezesha Hispania kutetea taji lao.
Iniesta alitegeneza bao muhimu lililofungwa na Jesus Navas
likiwa ni bao pekee dhidi ya Croatia kwenye mchezo wa mwisho wa makundi,
huku pasi yake nyingine kwa Cesc Fabregas katika mchezo wa fainali
ikimsaidia Fabregas kupiga krosi iliyomkuta David Silva aliyefunga bao
la kwanza.
Katika tuzo hiyo Iniesta alifanikiwa kuwapiku Andrea
Pirlo wa Italia na nyota mwezake wa Barcelona, Xavi aliyetwaa tuzo hiyo
mwaka 2008.
Iniesta amekuwa miongoni mwa wachezaji 10 wa Hispania wanaounda kikosi cha wachezaji 23 wa mashindano hayo.
Naye mshambuliaji wa Hispania, Fernando Torres amefanikiwa kutwaa Kiatu cha Dhahabu kufuatia kuibuka mfungaji bora na kumpiku mwenzake wa Ujerumani,Mario Gomez.
Naye mshambuliaji wa Hispania, Fernando Torres amefanikiwa kutwaa Kiatu cha Dhahabu kufuatia kuibuka mfungaji bora na kumpiku mwenzake wa Ujerumani,Mario Gomez.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28, alifunga
bao moja katika ushindi wao wa mabao 4-0 dhidi ya Italia na kumfanya
kuwa mchezaji pekee aliyefunga mabao katika mechi mbili tofauti za
fainali.
Bao hilo lilimfanya kuwa sawa na Gomez aliyefunga mabao matatu na kutegeneza bao moja kwenye michuano hiyo iliyofikia tamati jana.
Hata hivyo, Uefa iliamua kumpa Torres zawadi hiyo kutokana na kutumia muda mchache uwanjani na kufunga mabao.
Nyota huyo wa Hispania alitumia dakika 189 kucheza mashindano hayo kulinganisha na Gomez aliyetumia dakika 280.
Wachezaji wengine wanne waliofunga mabao matatu ni Mario Balotelli (Italia), Cristiano Ronaldo (Ureno), chipukizi wa Russia, Alan Dzagoev na nyota wa Croatia, Mario Mandzukic.

Tuzo hiyo inamfanya Torres kumaliza
vizuri zaidi msimu wa 2011/12 baada ya kutwaa Kombe la FA na Ligi ya
Mabingwa akiwa na klabu yake ya Chelsea, lakini ameshindwa kuingia
kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa michuano ya Euro 2012 kilichotajwa
jana na Uefa.
Hispania imekuwa timu ya kwanza ya taifa kutwaa
mataji matatu mfululizo tangu, Euro 2008, Kombe la Dunia 2010 na Euro
tena mwaka huu.
إرسال تعليق