![]() |
| Kampteni Komba akiwa na mkewe, Salome Komba nyumbani kwake Kawe leo |
Mkurugenzi wa Kundi la
Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi,
Kapteni mstaafu, John Komba amerejea kutoka India ambako amefanyiwa
upasuaji kumtibu ugonjwa wa nyonga ulilokuwa ukimsumbua upande wa mguu
wake wa kulia.
Akizungumza na waandishi wa
habari, leo, Julai 27, 2012, nyumbani kwake Mbezi, Kawe, Dar es Salaam,
Komba alisema amerejea nchini, Juzi, baada ya kupatiwa matibabu hayo
kwenye hospitali ya Appolo iliyopo Hydrabad nchini India tangu mwanzoni
mwa wezi huu.
Alisema, aliondoka nchini, Julai
2, 2012, baada ya kupelekwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Jakaya
Kikwete, Spika wa Bunge Anna Makinda na Katibu wa Bunge John Kashilila
na kwamba alikwenda baada ya kukosa matibabu hapa nchini kwa sababu ya
mgomo wa madaktari.
"Siku napelekwa Muhimbili tu,
tayari madaktari walikuwa wameanza siku ya kwanza ya mgomo wao, nikawa
sina namna ila kuujulisha uongozi wa Bunge na kisha nikamuomba
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, naye kwa mamlaka yake
akanisaidia haraka kama ambavyo huwasaidia wengine kwenda kutibiwa nje",
alisema Komba.
Alisema, uzito ulichangia sana
kusababisha mifupa kusagana kwenye nyonga upande wa mguu wa kulia,
ambapo hadi anakwenda India alikuwa na uzindo wa kilo 138 wakati wastani
wa uzito aliotakuwa kuwa nao kulingana na ukumbwa wa mwili wake ni kilo
90 au 100 tu.
"Amesema, baada ya matibabu
amerejea nchini akiwa na uzito wa kilo 128 ambao hata hivyo ametakiwa
kuudhibiti na kuupunguza katika siku hizi ambazo atalazimika kupumzika
nyumbani kabla ya kuanza kazi, Mwezi Septemba mwaka huu kama
alivyoelekezwa na madaktari.
Akizungumzia upasuaji
ulivyoendeshwa, Komba alisema, ulichukua saa tano na kukamilika bila
matatizo katika upasuaji huo ambao alisema sehemu iliyopasuliwa ni ya
ukumbwa wa futi moja.
Alisema, hata hivyo baada ya
upasuaji huo, hakuweza kurejea katika wodi ya kawaida, kwa sababu
majongwa kadhaa yaliibuka ikiwemo homa kali, presha, hivyo akalazimika
kulazwa katika wodi ya wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU)
kwa siku tano.
"Sasa nimerejea nikiwa mzima,
kwa sasa natumia fimbo hii, ili kuwezesha uzito uzilemee upande wa kulia
nilikopanyiwa upasuaji, lakini sijambo kabisa", alisema Komba.
Komba alilaani baadhi ya vyombo
vya habari ambavyo viliripoti kwamba katika kuugua kwake alikuwa
mahututi na kwamba alikuwa anaugua figo.
"Jamani ninyi waandishi wa
habari, jizoesheni kuandika habari zilizokamilika siyo kurashia-rashia
tu na kuzusha uongo, mfano gazeti moja liliandika eti naugua figo nipo
mahututi, wakati si kweli kabisa, ilikuwa jambo rahisi tu, kuja hapa
nyumbani na kuniuliza au kuuliza mke wangu lingepata kwa uhakika
ninachoumwa", alisema Komba.
Chanzo:- TANZANIA VISION BLOG

Post a Comment