Kiiza ajigamba, Tegete matatani Yanga

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Hamis Kiiza amejisifu kwa kufunga penalti ya staili ya 'panenka' katika mchezo wa robo fainalu ya Kombe la Kagame dhidi ya Mafunzo kwa kusema ni utaalamu alioupata baada ya kuufanyia mazoezi na si kwamba alibahatisha.

Panenka ni staili adimu na maarufu duniani ya upigaji wa penalti, ambapo mpigaji hupiga mpira kwa staili ya kuuchopu mpira na mara zote makipa wamekuwa 'wakiuzwa' hivyo kushindwa kuokoa mchomo usiguse nyavu zao.

Staili hii  ilipewa jina la Panenka  kama heshima ya kumuenzi mwasisi wake, mchezaji wa zamani wa Jamhuri ya Czech Antonin Panenka ambaye katika fainali ya Michuano ya Ulaya ya mwaka 1976 dhidi ya Ujerumani alifunga penati ya ushindi kwa kwa kuuchopu mpira juu kidogo katikati ya goli huku kipa akiruka upande mwingine.

Akizungumza baada ya mchezo huo kwa  Yanga kuishinda Mafunzo kwa penati 5-4, Kiiza alisema hakuwa na wasiwasi wakati akienda kupiga penalti  ya aina hiyo kwakua kabla ya mechi hiyo alishaifanyia mazoezi ya kutosha na kufunga.

"Ukweli ni kwamba, upigaji huu wa penalti nimeufanyika mazoezi, nilijua nitafunga kama ambavyo kule kwenye mazoezi yetu nimekuwa nikifanya, sikubahatisha," alisema Kiiza mwenye mabao manne kwenye michuano hiyo mpaka sasa.

Staili hiyo ya kuvutia ya kupiga penati pia ilishuhudiwa ikitumiwa na kiungo wa Italia, Andrea Pirlo pamoja na beki wa Hispania, Sergio Ramos kwenye michuano ya Uero 2012  iliyomalizika mwanzo mwa mwezi huu.

Wakati huohuo; Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet ameeleza kutolizishwa na kiwango cha mshambuliaji wake Jerryson Tegete na kumtaka abadilike kama anataka kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

"Kama wakishindwa kubalika na kukubaliana na ninayowataka wafanye itabidi watupishe kwa kuwatoa kwa mkopo katika timu nyingine na wengine watafute sehemu za kwenda," alisema Saintfiet huku akimtolea mfanoTegete.

Alisema Tegete amekuwa haonyeshi kujituma uwanjani kila anapopewa nafasi tofauti na wenzake Kiiza na Said Bahanuzi.

Alisema kama mchezaji huyo hataki kubadilika na kucheza kwa kujituma kama wenzake basi haitokuwa tatizo kwake kumwacha kwa faida ya timu.

Kauli hiyo ya Saintfiet inaungana na ile aliyowahi kuisema Kostadin Papic kwamba uwezo wa Tegete umeshuka na kumtaka abadilika.

Post a Comment

Previous Post Next Post