
Mabingwa
wa Soka Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam leo imekubali
kichapo cha goli 3-1 kutoka kwa wapinzani wao wa sasa Azam ambao ni
washindi wa pili wa Ligi Kuu, katika mchezo wao wan ne wa Robo fainali
ya kombe la Kagame 2012.
Azam
kwa ushindi huo sasa imetinga nusu fainali na kwa soka la uhakika
walilotandaza hii leo wanamatumaini makubwa wa kunyakua Kombe hilo kwa
mara ya kwanza iwapo itafanikiwa kuingia fainali kwa kuifunga AS Vita
kutoka Burundi.
Mbali na Azam na Vita timu nyingine zitakazo chuano katika Nusu fainali ni Yanga na APR .
Magoli
ya Azam leo yalipachikwa kiamini na Mpachika Mabao namba moja wa Ligi
Kuu John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyepachika wavuni magoli hayo huku
moja kipindi cha kwanza na mawili katika kipindi cha pili.
Bocco alipachika goli la kwanza dakika ya 17 na kupachika mengine mawili katika dakika ya 46 na msumari wa mwisho dakika ya 73.
Goli la Simba lilifungwa na Shomari Kapombe aliyetokea nyuma na kupeleka mashambuzi langoni mwa Azam na kuzaa matunda.
Vikosi vya leo ni kama hivi
Azam FC; Deo
Munishi, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris,
Kipre Michael Balou/Ramadhan Chombo, Kipre Herman Tcheche/George
Odhiambo ‘Blackberry’, Salum Abubakar, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo na
Khamis Mcha ‘Vialli’/Jabir Aziz.
Simba SC; Juma
Kaseja, Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino Masombo, Juma Nyosso,
Mussa Mudde, Uhuru Suleiman/Kiggi Makassy, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu,
Haruna Moshi na Jonas Mkude/Amri Kiemba.
Post a Comment