MISS UTALII KAGERA NI IRENE BWIRE


MISS UTALII KAGERA 2012 MISS IRENE BWIRE KATIKATI NA MSHINDI
WA PILI MISS JANIA ABDUL KUSHOTO NA MISS MAYOR KASHUMBA MSHINDI WA
TATU KULIA.

Mrembo Irene Bwire, mwishoni mwa wiki ameibuka mshindi wa Taji la Miss
Utalii Kagera 2012, katika shindano lililofanyika katika ukumbi wa
Rinas Club mjini Bukoba mkoani kagera siku ya jumamosi tarehe
14-7-2012. Irene alitwaa taji hilo kwa kuwashinda warembo wengine 14,
katika shindano ambalo mkuu wa Wilaya ya Bukoba mama Pangani alikuwa
mgeni rasmi. Mrembo Jania Abdul alikuwa mshindi wa pili na Mayor
Kashumba alikuwa mshindi wa tatu, hivyo wote pamoja na mshindi wa
nne,watano na mshindi wa taji la Miss Utalii Vipaji watawakilisha mkoa
wa kagera katika fainali za Miss Utalii Tanzania 2012- Kanda ya
Magharibi,zitakazo fanyika mkoani Mara mwezi Oktoba 2012.


Katika shindano hilo ambalo lilisindikizwa na burudani za muziki wa

asili na wa kizazi kipya ikiwemo bendi ya Diamond Sound pamoja na msanii BK
Sanday  na makundi ya ngoma za asili za mkoa wa kagera, shindano hilo
liliandaliwa na Dinner Fashion,huku Miss Utalii Kilimanjaro 2012
Evamary Gamba akiwa ni mwalimu wa warembo.


Mgeni rasmi , mkuu wa wilaya ya Bukoba aliwapongeza waandaaji kwa

kufanikiwa kuaandaa shindano hilo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa ni
kichocheo cha kutangaza utalii na utamaduni wa mkoa wa Kagera. Aidha
alisema kuwa serikali na mkoa wa Kagera wanathamini sana mchango wa
shindano hilo katika kuhamasisha na kutangaza utalii na utamaduni wa
Tanzania pia mianya ya uwekezaji, na kuwataka wadau mbalimbali
kuliunga mkono kwa kudhamini shindano hilo kila linapofanyika

Post a Comment

أحدث أقدم