MKUTANO wa kujadili ukuaji wa demokrasia Afrika unaanza leo jijini Dares
Salaam, huku nchi 11 zikitarajiwa kushiriki.Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo
cha Demokrasia Tanzania ( TCD), James Mbatia alisema mkutano huo
utajadili misingi ya kisheria inayoongoza vyama vya siasa barani
Afrika.
Alisema: “ Lengo la mkutano huu ni kujadili misingi ya kisheria inayoongoza vyama vya siasa hasa kwenye kuviwezesha kiuchumi na vitendea kazi ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa masilahi endelevu.”
Alizitaja nchi zinazoshiriki katika mkutano huo kuwa ni Sudan Kusini, Ghana, Mali, Uganda, Kenya, Msumbiji, Zimbabwe, Burundi, Malawi, Tunisia na mwenyeji Tanzania.
Alisema mkutano huo umewezeshwa na Taasisi ya Demokrasia ya vyama vingi ya nchini Uholanzi (NIMD) pamoja na Asasi ya Kimataifa inayoshughulika na Demokrasia na Huduma za Uchaguzi(Idea).
Kwa mujibu wa Mbatia, mkutano huo utahusisha vyama tawala na vile vya upinzani kutoka nchi shiriki vikijadili mambo mbalimbali ikiwemo kuepukana na migogoro inayojitokeza baada ya kufanyika kwa uchaguzi katika nchi za Afrika.
Katika hatua nyingine, Mbatia alisema demokrasia nchini Tanzania kwa sasa imeimarika kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka 20 iliyopita kutokana na mwamko wa wanajamii na kusisitiza ukuaji huo uende sambamba na uchumi.
“Zamani ilikuwa ni ngumu kukuta majadiliano kama haya, lakini hatua tuliyofikia ya kujadiliana kuhusu Katiba Mpya ni jambo la kujivunia kwa Watanzania kutokana na ukomavu wao kidemokrasia,” alisema

إرسال تعليق