ALIYEKUWA mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Rose Kamili Slaa nee Sukum, amefungua kesi ya madai katika
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiiomba izuie Dk. Willibrod Slaa,
asifunge ndoa na mchumba wake, Josephine Mushumbusi.
Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo ya masuala ya ndoa iliyopewa
na Na. 4/2012 ambayo gazeti hili inayo nakala yake, ambayo tayari
imepangwa kusikilizwa na Jaji Laurence Kaduri, ilifunguliwa mahakamani
hapo hivi karibuni na wakali wa mlalamikaji Joseph Thadayo.
Washitakiwa katika kesi hiyo ni Dk. Slaa na mchumba wake, Josephine,
ambapo mlalamikaji anaiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe
kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa kwa ajili ya kupatanishwa.
Katika dai la pili, Rose anaiomba Mahakama itangaze kuwa yeye na Dk.
Slaa bado ni wanandoa na dai la tatu anaiomba itamke kuwa ndoa baina
yake na Dk. Slaa bado ni halali kisheria na kwamba ndoa nyingine
itakayofungwa kinyume cha sasa itakuwa ni batili.
Katika dai lake la nne, mlalamikaji ambaye sasa ni Mbunge wa Viti
Maalumu (CHADEMA), anadai kuwa Josephine, alimshawishi mumewe (Dk. Slaa)
kuivuruga ndoa yao.
“Pia nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga ndoa Julai 21 mwaka
huu, katika eneo lolote lile, ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili.
“Pia naiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wanilipe fidia ya sh milioni 50
kama gharama za matunzo ya watoto wawili, Emiliana na Linus aliyezaliwa
mwaka 1987,” alisema.
Rose anadai kuwa walianza kuishi pamoja na Dk. Slaa kama mume na mke,
na amekuwa akiwahudumia watoto hao peke yake tangu mwaka 2009 baada ya
Dk. Slaa kumkimbia.
Pia anaiomba mahakama imwamuru Josephine naye amlipe fidia ya sh
milioni 500 kwa sababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia
ndoa yake
Chanzo:- Tanzania Daima
Post a Comment