ALEX Ferguson yuko mjini London na huenda akatumia fursa hiyo
kumshawishi mshambuliaji 'aliyeikataa' Arsenal, Robin van Persie kwenda
Manchester United.
Bosi huyo wa United anatarajia kuwa mmoja wa
wageni waalikwa kwenye sherehe ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na
Labour Party Sports kwenye Uwanja wa Emirates.
Habari za ndani,
zinadai kuwa Fergie bado ana ndoto ya kumshawishi Van Persie kwenda
United hasa baada ya Madachi huyo kukataa kusaini mkataba mpya Arsenal.
United
itashindana na hasimu wake mkubwa kwenye Jiji la Manchester, klabu ya
Man City ambayo kwa muda mrefu imetajwa kumtaka nyota huyo.
Man
City inajiandaa kumpunguza mzigo wa washambuliaji wake kwa kumruhusu
Emmanuel Adebayor kusaini mkataba wa kudumu Spurs anakocheza kwa mkopo
kwa sasa.
Van Persie, anaonekana kufaa kucheza mfumo wa kocha wa City, Roberto Mancini ambao unatoa fursa kwa washambuliaji kuzunguka.
Kocha Fergie angependa kuona Van Persie akicheza sambamba na Wayne Rooney kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Van
Persie anataka suala lake Arsenal kumalizwa kabla ya klabu hiyo kuanza
ziara ya maandalizi ya Ligi Kuu barani Asia, Julai 24 mwaka huu.
United inaondoka Jumatatu ijayo kwenda Afrika Kusini kwa ziara kama hiyo na kisha pia kusimama Shanghai, China.
Wakati
huohuo, Kocha Arsene Wenger amewaambia maofisa wa Arsenal kuharakisha
kumalizika suala la Robin van Persie hata kama uamuzi ni kumuuza.
Wenger anatarajia kukutana ana kwa ana na Van Persie siku chache zijazo kwa lengo la kumshawishi kubaki Emirates.
Lakini kama atashindwa kufikia naye makubaliano, basi anataka auzwe haraka
Post a Comment