NGORONGORO WAPINGWA 2 MTUNGI DHIDI YA NYIGU
![]() |
| Michelsen, kocha wa Ngorongoro |
TIMU ya taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 20,
Ngorongoro Heroes, jana imefungwa 2 - 0 na Rwanda kwenye Uwanja wa Chamazi, katika
mchezo wa kirafiki, kujiandaa na mechi dhidi ya Nigeria Julai 29, kuwania
tiketi ya kucheza Fainali za Afrika.
Rwanda ‘Nyigu Wadogo’, waliowasili Dar es Salaam jana mchana kwa ndege ya shirika la ndege la Rwanda kwa ajili ya mechi mbili
za kirafiki dhidi ya Ngorongoro Heroes, leo waliizidi uwezo Ngorongoro.
Rwanda yenye msafara wa watu 27 wakiwemo wachezaji 20, ambayo
imefikia katika hoteli ya Sapphire, baada ya ushindi huo wa jana, itarudiana na
Ngorongoro kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ngorongoro Heroes iko kambini chini ya Kocha wake, Mdenmark Jakob
Michelsen na msaidizi wake Mohamed Adolf Rishard.
Mechi dhidi ya Nigeria ambayo ni ya kwanza ya raundi ya pili
kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini
Algeria itachezwa Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

إرسال تعليق