NITATATUA TATIZO LA MAGOLI STARS - POULSEN ANIITE TU:- BAHANUZI:
Top Scorer wa michuano ya Kombe la Kagame, Said Bahanunzi wa Yanga amesema kwa sasa anafikiri ni wakati wake kuitwa kikosi cha timu ya Taifa Stars.Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Yanga akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
"Nafikiri kwa sasa tuna tatizo la ufungaji timu ya taifa, naamini nitakapopewa nafasi nitaendeleza haya niliyofanya Kagame na timu kupata ushindi."Aliongeza: "Siri yangu kubwa kuibuka mfungaji bora ni kwa sababu nilimtanguliza Mungu mbele kwa kila jambo na kujituma."
"Nimezaliwa na kulelewa katika mazingira ya dini, ninamwamini zaidi mwenyezi Mungu kuliko chochote."
"Sidhani kama kweli kuna uchawi kwenye soka, ni imani potofu za watu wachache, nimejipanga kufanya vizuri zaidi na siyo kuishia hapa."
"Kila jambo nalofanya namtangulia Mungu, nafikiri ndiyo siri kubwa yangu kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame.
Aliongeza kusema ushirikiano kati yake na wachezaji ulimsaidia kujiona yuko nyumbani na kujituma zaidi.
Bahanunzi alishawahi kuichezea Ocean View ya Zanzibar na Mtibwa Sugar ya Morogoro kabla ya kutua Yanga msimu huu.
Source:Mwananchi
إرسال تعليق