ROBO FAINALI COPA COCA-COLA 2012
Robo
Fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inayokutanisha vijana wenye
umri chini ya miaka 17 inaanza kesho (Julai 10 mwaka huu) kwa timu nne
kuumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salam.
Temeke
na Mjini Magharibi ndizo zitakazocheza robo fainali ya kwanza kuanzia
saa 2.30 asubuhi. Mara iliyoivua ubingwa Kigoma itacheza robo fainali ya
pili dhidi ya Morogoro kwenye uwanja huo huo.
Robo
Fainali ya tatu itachezwa keshokutwa (Julai 11 mwaka huu) kwa
kuzikutanisha timu za Kinondoni na Mwanza. Mechi hiyo itaanza saa 2.30
asubuhi na kufuatiwa na nyingine kati ya Dodoma na Tanga itakayoanza 10
kamili jioni.
Nusu
fainali ya michuano hiyo iliyoanza Juni 24 mwaka huu katika mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani ikishirikisha timu 28 itafanyika Julai 13 mwaka
huu kwenye uwanja huo huo.
Mshindi
wa mechi kati ya Temeke na Mjini Magharibi, na Kinondoni dhidi ya
Mwanza ndiyo watakaocheza nusu fainali ya kwanza. Nusu fainali ya pili
itakuwa mshindi wa mechi ya Mara na Morogoro dhidi ya mshindi wa mechi
ya Dodoma na Tanga.
Fainali
itafanyika Jumapili (Julai 15 mwaka huu). Mechi zote kuanzia hatua ya
robo fainali hadi fainali zitafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume


إرسال تعليق