Wabunge
wakiendelea na kikao cha Bunge Bungeni ambapo jana ilimlazimu mbunge wa
Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi) Moses Machali kutolewa nje ya kikao hicho
MBILINYI AFANANISHA WALIOMTEKA NA JANJAWEED, WAZIRI NAGU AINGILIA KATI
Waandishi Wetu
KITENDO cha kutekwa nyara, kuteswa na kisha kuumizwa mwili mzima, kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka jana kilitikisa Bunge huku wabunge wa CCM na Chadema wakitupiana mpira kuhusu nani waliohusika na tukio hilo.

Msuguano huo ulianza baada ya
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi kudai kuwa waliofanya
kitendo hicho ni sawa na wanamgambo hatari wa Janjaweed wa Sudan.
Kauli
hiyo ya Mbilinyi maarufu kwa jina Sugu, ilizusha tafrani ndani ya Bunge
kwani Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji), Dk Mary Nagu
aliomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, Sylivester Mabumba aliyekuwa
akiendesha Bunge jana jioni akihusisha matamshi hayo na kuituhumu
Serikali kutumia watu kama Janjaweed katika kumteka Dk Ulimboka jambo
ambalo alisema siyo la kweli.
Akichangia Hotuba ya Ofisi ya Rais,
(Utumishi, Utawala Bora, Ikulu na Mipango) Mbilinyi alisema kitendo
alichofanyiwa Dk Ulimboka ni cha kinyama na baadhi ya watu wanaamini
kwamba Serikali ilihusika, hatua ambayo ilimfanya Dk Nagu kusema
Mbilinyi alikuwa akizungumzia jambo ambalo hana uhakika nalo na kutaka
aamriwe kuthibitisha.
Mwenyekiti Mabumba alimtaka Mbilinyi
athibitishe kauli yake au aifute. Wakati Mabumba akimtaka Mbilinyi
kuthibitisha au kufuta kauli yake, Mbunge wa Singida Mashariki
(Chadema), Tundu Lissu alitaka kuingilia kati suala hilo na hata kuwasha
kinasa sauti, lakini Mabumba alimwamuru akae chini.
Mbilinyi
alipopewa nafasi alisisitiza: “Waliomteka Dk Ulimboka walikuwa na silaha
kama siyo askari, basi hawana tofauti na kikundi cha Janjaweed ambacho
kilifanya mauaji makubwa na kumfanya Rais wa Sudan, Omar Al Bashir
ambaye sasa anatakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai kuhusu
kufanya uhalifu dhidi ya binadamu.”
Alifafanua kwamba, hakusema
kama Serikali inatumia Janjaweed, bali alizungumzia namna Al Bashir
alivyotumia wapiganaji hao kufanya uhalifu badala ya jeshi.
Hali
hiyo ilizidi kuzua mvutano kati ya kiti cha Spika na Mbilinyi uliodumu
kwa dakika tatu, huku Lissu naye akitaka apewe nafasi atoe hoja yake.
Baadaye
Mabumba alitumia busara na kuamua kumalizia suala hilo kwa kumtaka
Mbilinyi aendelee kuchangia na mbunge huyo wa Mbeya akiendelea
kuzungumzia zaidi hilo, alitaka Bunge liunde tume ya uchunguzi kwa
sababu hana imani na Serikali kuunda tume kuchunguza ukatili huo.
Baada
ya Mbilinyi kumaliza, Mabumba alimtaka Lissu atoe dukuduku lake na
aliposimama alimpinga Mwenyekiti huyo wa Bunge kwa maelezo kwamba
alitumia kifungu kisicho sahihi kumwamuru Mbilinyi atoe maelezo ya
kuthibitisha au kufuta kauli. Hata hivyo, alimtaka akae chini akisema:
“Usitafute umaarufu hapa.”
Baadaye alisimama Mbunge wa Viti
Maalumu (CCM) Stella Manyanya ambaye alikituhumu Chadema kwa kuchochea
mgomo huku akidai kwamba kilihusika kumteka na kumjeruhi Dk Ulimboka.
Mbunge
wa Ubungo (Chadema), alikuja juu baada ya kauli hiyo akimtaka
Mwenyekiti amtake Manyanya kuthibitisha au kufuta kauli yake. Badala
yake, Mabumba alimtaka Mnyika kuthibitisha kwamba chama hicho
hakihusiki.
Mnyika alisema Chadema hakihusiki na suala hilo na
kueleza kwamba ripoti ya Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza mgogoro
wa madaktari na Serikali inathibitisha hivyo, akitaka iwasilishwe
bungeni na isomwe.
Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu
Nchemba alisema Chadema kinaunga mkono mgomo wa madaktari akirejea
hotuba ya upinzani bungeni iliyotolewa jana ikisema inawaomba wananchi
kwa kushirikiana na madaktari kuiunga mkono Chadema kuishinikiza
Serikali hadi wapate haki zao.
Manyanya alisimama tena na kudai
kwamba hata waliomteka daktari huyo walikuwa wamevaa magwanda ambayo
yanatumiwa na makada wa Chadema kauli ambayo iliibua mzozo huku wabunge
wengi wa Chadema wakisimama kutaka kuzungumza.
Mwenyekiti Mabumba
alilazimika kutumia dakika kadhaa kuwataka wabunge watulie na wakae
chini lakini Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali
alikataa kutii amri hiyo akitaka kuzungumza hali ambayo ilimfanya
Mabumba kuamuru atolewe nje ya eneo la Bunge na kumtaka Manyanya
aendelee kuzungumza.
Muhimbili utata mtupu
Wakati uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ukisema huduma katika hospitali hiyo zimerejea katika hali ya kawaida baada ya madaktari kurejea kazini jana, madaktari bingwa wa hospitali hiyo nao wametangaza kuanza mgomo.
Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa uongozi wa Muhimbili, Aminiel Aligaesha imesema wagonjwa wote waliolazwa wodini jana walihudumiwa na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika na kuongeza: “Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji.”
Lakini wakati uongozi wa Muhimbili ukisema hivyo, madaktari bingwa walikutana jana katika hospitali hiyo na kutangaza kuanza mgomo. Akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika katika hospitali hiyo, msemaji wao Dk Catherine Mng’ongo alisema:

“Sisi madaktari bingwa
kufanya kazi bila Interns haiwezekani. Tungeanza kufukuzwa sisi kwanza.
Kuanzia sasa hatutafanya kazi hadi hapo Serikali itakapokubali
kuwarejesha wote kazini na kufungua meza ya majadiliano yenye nia ya
dhati ya kumaliza mgogoro.”
Dk Mng'ong'o alisema zaidi ya
madaktari 200, waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo Muhimbili na Taasisi
ya Mifupa (Moi) wamepatiwa barua za kufukuzwa kazi na idadi yao nchi
nzima inafikia 300.
Tamko la Rais Kikwete
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania , Dk Godbles Charles ameeleza kushangazwa na kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa Serikali haihusiki katika sakata hilo na akidai ameingilia kazi ya tume iliyoundwa na Polisi kuchunguza tukio hilo.

“Je, ni sahihi kwa
Rais kutamka waziwazi kuwa Serikali yake haihusiki kwa namna yoyote ile
hata kabla ya ripoti ya uchunguzi?” alihoji Dk Charles.
Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa hali ya Dk Ulimboka inaendelea vizuri anakotibiwa Afrika ya Kusini.
Hospitali nyingine
Madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC wamekubaliana na kuendelea na mgomo wakisubiri uamuzi wa mkutano mkubwa wa madaktari utakaofanyika leo.
Madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC wamekubaliana na kuendelea na mgomo wakisubiri uamuzi wa mkutano mkubwa wa madaktari utakaofanyika leo.
Jumamosi
iliyopita, uongozi wa KCMC uliwatimua madaktari zaidi ya 80 walioko
kwenye mafunzo kwa vitendo na kuwataka wasionekane katika eneo la
hospitali wala kukusanyika hapo.
Uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, umelazimika kuitisha kikao cha pamoja na madaktari wa hospitali hiyo kwa lengo la kuwasihi waachane na mgomo.
Vyanzo vya habari hospitalini hapo, vilidai ya kwamba katika kikao hicho uongozi wa hospitali hiyo chini ya Mganga Mkuu Mfawidhi, ulilazimika kuitisha kikao siku moja baada ya tukio la Dk Ulimboka na kuwaangukia madaktari hao waachane na mgomo.
Huko Mbeya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk Eliuter Samky amesema utoaji huduma kwa wagonjwa siyo wa kuridhisha kutokana na kuathirika kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya sekta muhimu.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, Samky alisema mgomo huo umesababisha kuzorota kwa huduma kwa wagonjwa licha ya kusitisha huduma nyingine za kawaida na kubaki kuendelea kutoa huduma za dharura.

Chanzo:- http://mwananchi.co.tz
إرسال تعليق