Simba yamtimua mrithi wa Yondani


 SIMBA imewatema nyota wake watatu akiwamo beki Lino Masombo baada ya kuboronga kwenye mashindano ya Kombe la Kagame.

Habari ambazo http://www.mwanaspoti.co.tz limezinasa zinaeleza uongozi wa Simba ulikaa wikiendi iliyopita na kufikia uamuzi huo mgumu.

Masombo anayeaminiwa alichukuliwa kuziba pengo la Kelvin Yondani aliyetimkia Yanga, ndiye anayeongoza orodha ya kutimuliwa akiwa na Salum Kinje na Haruna Shamte.

Kinje alisajiliwa kutoka AFC Leopards ya Kenya wakati Shamte alirudishwa kikosini baada ya kutolewa mkopo kuchezea Villa Squads kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu uliopita.

Masombo alisajiliwa kutoka Motema Pembe ya Congo, hata hivyo ameshindwa kuonyesha makali yake kwenye Kombe la Kagame.

"Jamaa wamepigwa panga baada ya kuonyesha kiwango cha chini katika michuano ya Kagame," alisema mtu mmoja, ambaye yuko karibu na uongozi wa klabu hiyo.

Pamoja na kuwatimua wachezaji hao, nyota wengine Uhuru Selemani, Danny Mrwanda na Kanu Mbiyavanga wamepewa onyo kali kwa kucheza chini ya kiwango.

Mmoja wa wachezaji wanaotakiwa kutimuliwa, Kinje aliiambia Mwanaspoti kuwa anaendelea na mazoezi.
Hata hivyo, uongozi wa Simba kupitia kwa Ofisa Habari, Ezekiel Kamwaga alisema: "Upo uwezekano wa wachezaji walionekana katika michuano ya Kagame wasiwepo katika usajili wetu kutokana na sababu mbalimbali.

"Wapo wachezaji waliocheza mashindano yale kwa mapatano bila mkataba, tunaweza kumalizana nao lakini siwezi kuwataja majina."

Simba ilitolewa katika robo fainali ya Kombe la Kagame ilionyesha udhaifu mkubwa katika beki yake.

Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic, alishindwa kupata kombinesheni nzuri na alilazimika kuwabadilisha mara kwa mara, Shomari Kapombe, Obadia Mungusa, Juma Nyosso, Masombo na Shamte.

Klabu hiyo ilipata pigo zaidi baada ya Amir Maftah kuumia

Post a Comment

أحدث أقدم