SIKU moja tangu serikali kutangaza nyongeza ndogo ya mishahara ya
kima cha chini kwa watumishi wa umma ,Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Nchini (TUCTA) limepinga mshahara huo.
Akizungumza na Tanzania Daima jana Katibu Mkuu wa shirikisho hilo
Nicholaus Mgaya alisema wao tangu mwaka 2006 wamekuwa wakiishauri
serikali kuweka kima cha chini cha 315,000 lakini hakuna utekelezaji
wake hadi leo.
Alisema kutokana na hotuba iliyosomwa juzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) wameifuatilia kwa makini wameona
kuwa hakuna jipya zaidi ya serikali kuendelea kuwakandamiza watumishi na
kuwagawa kwa walionacho na wasionacho.
Alisema kwa mfanyakazi wa kima cha chini na yule anayepokea shilingi
mil. tatu na nne wakikatwa bado wa sh mil. 4 anabaki kuwa juu zaidi ya
yule wa kima cha chini kiasi kwamba wataendelea kutaabika na kunyonyeka
huku uendeshaji wa maisha kwa sasa ukiendelea kuwa mgumu.
Mgaya alisema hata hivyo wamesikiasikia kuwa kima cha chini cha
mshahara kitakuwa sh 170,000 lakini wanangoja kwa hamu kitangazwe rasmi
ili nao waweze kutoa maamuzi yao mara baada ya kupitia.
“Haki haijatendeka na kuwa tofauti kubwa kwa waliopo chini watabaki
kuwa chini na wa juu watabaki kuwa juu sasa tunakaa na kufikiri tuone
tufanye nini wakati tukiendelea kuipitia zaidi na zaidi,” alisema Mgaya.
Mgaya pia alisema madai mengine waliiomba serikali kupunguza gharama
za tozo za mifuko ya hifadhi ya jamii, ili wafanyakazi wa kima cha chini
waweze kumudu maisha ambayo kwa mshahara mdogo walionao hawawezi kumudu
maisha hayo
Chanzo:- Tanzania Daima
Post a Comment