TUCTA yapinga nyongeza mpya ya mishahara

SIKU moja tangu serikali kutangaza nyongeza ndogo ya mishahara ya kima cha chini kwa watumishi wa umma ,Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) limepinga mshahara huo.
Akizungumza na Tanzania Daima jana Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Nicholaus Mgaya alisema wao tangu mwaka 2006 wamekuwa wakiishauri serikali kuweka kima cha chini cha 315,000 lakini hakuna utekelezaji wake hadi leo.
Alisema kutokana na hotuba iliyosomwa juzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) wameifuatilia kwa makini wameona kuwa hakuna jipya zaidi ya serikali kuendelea kuwakandamiza watumishi na kuwagawa kwa walionacho na wasionacho.
Alisema kwa mfanyakazi wa kima cha chini na yule anayepokea shilingi mil. tatu na nne wakikatwa bado wa sh mil. 4 anabaki kuwa juu zaidi ya yule wa kima cha chini kiasi kwamba wataendelea kutaabika na kunyonyeka huku uendeshaji wa maisha kwa sasa ukiendelea kuwa mgumu.
Mgaya alisema hata hivyo wamesikiasikia kuwa kima cha chini cha mshahara kitakuwa sh 170,000 lakini wanangoja kwa hamu kitangazwe rasmi ili nao waweze kutoa maamuzi yao mara baada ya kupitia.
“Haki haijatendeka na kuwa tofauti kubwa kwa waliopo chini watabaki kuwa chini na wa juu watabaki kuwa juu sasa tunakaa na kufikiri tuone tufanye nini wakati tukiendelea kuipitia zaidi na zaidi,” alisema Mgaya.
Mgaya pia alisema madai mengine waliiomba serikali kupunguza gharama za tozo za mifuko ya hifadhi ya jamii, ili wafanyakazi wa kima cha chini waweze kumudu maisha ambayo kwa mshahara mdogo walionao hawawezi kumudu maisha hayo
Chanzo:- Tanzania Daima

Post a Comment

أحدث أقدم