Warwanda Mbuyu, Iranzi watajwa Yanga

BEKI wa APR ya Rwanda, Buyi Twite na kiungo wa timu hiyo Jean Claude  Iranzi wamehusishwa na mpango wa kujiunga na klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam tayari kukipiga msimu ujao.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kupitia mtandao mmoja nchini Rwanda, mikataba ya wachezaji hao wanaocheza APR ya Rwanda, inamalizika hivi karibuni.
Taarifa hiyo ilidai kuwa tayari Mbuyi na Iranzi wamefanya mazungumzo ya awali na Yanga ambayo imeonyesha nia ya kuwasajili.
Habari zaidi zilidai kuwa Yanga ipo tayari kutoa kitita cha Franc za Rwanda  18milioni kwa ajili ya kumnasa Twite na Franc 7milioni ili kumtwaa Iranzi.
Pia ilielezwa, mbali ya Iranzi kutakiwa na Yanga, klabu nyingine ya Rayon Sports ya Rwanda nayo imekuwa imetajwa kuwania saini ya nyota huyo.
Katibu Mkuu wa APR, Adolphe Kalisa amesisitiza kuwa mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati yao na wachezaji hao kuhusu kuongeza mkataba.
"Hatujafanya mazungumzo yoyote ya kuongeza mikataba na wachezaji hawa mpaka sasa, tumeamua kuacha kwanza mpango huu mpaka baada ya michuano ya Kombe la Amani itakapomalizika," alisema Kalisa.
Akizungumzia mpango huo, Iranzi  alikiri kufuatwa na Yanga lakini akasema aliomba apewe muda ili aweze kuelekeza akili yake kuisaidia APR kwenye michuano ya Kombe la Amani.
Mmoja wa waratibu wa usajili klabu ya Yanga, Seif Ahmed alipoulizwa kuhusiana na mpango huo, alisema hana lolote analofahamu.
Ahmed alisema taarifa hizo ni mpya kwake kwa vile hakuwahi kusikia mpango wowote wa kutaka kuwasajili wachezaji hao.
"Mimi nachofahamu ni kwamba, kulikuwapo na mazungumzo kati yetu na mshambuliaji wa Polisi ya Rwanda, Meddie Kagere," alisema Ahmed.
Kuhusu mazungumzo na Kagere, Ahmed alisema: "Mazungumzo yamefikia hatua nzuri, tunaelekea ukiongoni kumaliza mambo kabisa."
Wakati huohuo, Kamati ya Uchaguzi ya  Yanga imewataka wagombea watano wa nafasi za uongozi wa klabu hiyo kuwasilisha vyeti vyao halisi vya elimu kufikia saa 10 jioni leo ili vihakikiwe.
Wagombea hao ni  Sara Ramadhani anayewania nafasii ya Uenyekiti, Abdalah Mbara, Edgar Fongo, Ahmed Gau na Shaaban Katwila wanaofukuzia nafasi za ujumbe.
Akizungumza jana, Mwenyekiti wa kamati, John Mkwawa alisema wagombea hao wataondolewa kwenye orodha iwapo watashindwa kutimiza agizo hilo.
Mkwawa alisema kuwa hatua ya kamati yake kuwataka wagombea hao kuwasilisha vyeti hivyo inalenga kutekeleza agizo iliyopewa na Shirikisho la Soka Tanzania(TFF).
Aidha, Mkwawa alisema kampeni kwa wagombea wa uchaguzi huo zitaanza rasmi kesho na kuongeza kuwa wagombea wataruhusiwa kunadi sera zao kuanzia asubuhi na hadi saa 12

Post a Comment

Previous Post Next Post