BEKI wa zamani wa Simba, Salum Kanoni amejiunga na Kagera Sugar kwa mkataba wa miaka miwili.Kanoni amejiunga na timu hiyo ili kuziba pengo la David Lwende aliyetimikia Yanga msimu huu.
Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussen alisema taratibu zote za usajili wa mchezaji huyo zimekamilika na wakati wowote kuanzia sasa ataungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya kujiandaa na kivumbi cha Ligi Kuu.
"Ni kweli kabisa tumemsajili Kanoni ni matumaini yetu kuwa atatusaidia kutokana na uzoefu wake mkubwa alionao ukilinganisha na wachezaji wengine.
"Tuimeingia naye maktaba wa miaka miwili hiyo ndiyo nafasi yake ya kuhakikisha apigana kwa nguvu zake ili aweze kuandika historia ya mafanikio akiwa na klabu yetu," alisema Mohamed.
Katika hatua nyingine uongozi wa klabu hiyo unaendelea na zoezi la kutafuta kocha mpya atakayechukua mikoba ya Salum Mayanga aliyetimuka msimu huu baada ya kushindwa kuiongoza timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu msimu uliopita.
Wakati huo huo; Vita ya kuwania namba katika kikosi cha kwanza cha timu ya Yanga imeanza kuonekana baada ya Haruna Niyonzima kuanza mazoezi na wenzake ya kujiandaa na michuano ya Kagame.
Wachezaji wa timu hiyo hususani wale wanaocheza nafasi kiungo wanaongoza kwa kujituma zaidi mazoezini ili kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza.
Hali hiyo imefurahisha kocha msaidizi wa timu hiyo Felix Minziro ambaye anaamini itaisaidia kwenye michuano ya Kagame.
Minziro alisema benchi la ufundi la timu hiyo bado linakazi kubwa ya kuhakikisha linapata kikosi cha kwanza kutokana na wachezaji wote kuwa na uwezo mkubwa wa kutandaza soka.
"Vijana wanaushindani mkubwa na zaidi wale waocheza nafasi ya kiungo kwa hakika nafurahia hali hii kwani ni moja kati ya mambo muhimu yanayohitajika mazoezini
Post a Comment