Waziri
wa Maji, Prof Jumanne Maghembe akiwasilisha bungeni makadirio na
matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/13, mjini Dodoma jana.
Picha na Edwin Mjwahuzi
WIZARA
ya Maji jana iliwasilisha makadirio yake ya matumizi kwa mwaka
20012/2013 bungeni ambayo yanaonyesha kuwa imetenga Sh465.756 bilioni
kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Akiwasilisha bajeti hiyo, Waziri wa
Maji, Profesa Jumanne Maghembe alisema kati ya fedha hizo, Sh140.015
bilioni ni za ndani na Sh325.740 ni fedha kutoka nje.
Hata hivyo, Kambi ya Upinzani Bungeni katika hotuba yake, imeikosoa ikisema sekta ya maji inaendeshwa kwa kutegemea fedha za wafadhili na kwamba hali hiyo inaathiri utekelezaji wa miradi inayokusudiwa.
Profesa Maghembe alisema kwa ujumla wake, wizara yake inakusudia kutumia Sh485.898 bilioni, kati ya hizo matumizi ya kawaida ni Sh20.142 bilioni.
Alisema miongoni mwa kazi ambazo wizara hiyo imepanga kuzitekeleza ni pamoja na maeneo yanayofaa kuchimba visima virefu na kusimamia uchimbaji kwa maeneo 630 katika sehemu mbalimbali nchini.
“Mwaka 2012/2013, kupitia Bajeti ya Serikali, Sh51.9 bilioni kutoka mfuko wa pamoja zimepangwa kugharimia ujenzi wa miundombinu ya maji, kujenga uwezo wa watekelezaji wa programu, uhamasishaji, kutoa elimu ya usafi na mazingira, ufuatiliaji na kulipa wataalamu washauri kwa ajili ya usimamizi wa makandarasi,” alisema Profesa Maghembe na kuongeza:
“Kiwango hicho cha fedha kilichotengwa ni sehemu ya Sh81.8 bilioni ya mchango wa Serikali na ahadi ya Washirika wa Maendeleo.”
Alisema Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Dharura wa Kuboresha Huduma ya Maji katika Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha na Bagamoyo ambao unalenga kuongeza uwezo wa uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 300,000 kwa siku hadi mita za ujazo 710,000 siku ifikapo 2014.
Profesa Maghembe alisema mpango huo unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Serikali ya Norway, Serikali ya India na washirika wengine wa maendeleo kupitia Mfuko wa Pamoja wa Maji.
“Utekelezaji wa Mpango huo ulianza rasmi Februari 2011 na umepangwa kukamilika Desemba 2014 na utagharimu Sh653.9 bilioni,” alisema Profesa Maghembe. Alizitaja kazi zinazoendelea kutekelezwa kuwa ni ujenzi wa Bwawa la Kidunda, ambao usanifu wake ulianza 2010 na utakamilika Agosti, mwaka huu.
Alisema usanifu huo pia umejumuisha mtambo wa kuzalisha umeme wa megawati 20 na kwamba Sh3.4 bilioni zimetengwa kwa ajili ya ulipaji wa fidia kwa watu wanaoishi kuzunguka eneo la mradi.
Waziri Maghembe alisema sehemu nyingine ya mradi huo ni uchimbaji wa visima virefu vya Kimbiji na Mpera ambao utekelezaji wake haukuanza mwaka jana kama ulivyokuwa umepangwa kutokana na kuchelewa kwa taratibu za ununuzi.
“Kwa sasa zabuni za kuwapata makandarasi wa kuchimba visima vinane vya majaribio na visima 20 vya uzalishaji maji katika maeneo hayo zimetangazwa. Mikataba ya uchimbaji itasainiwa Septemba, 2012 na kazi kuanza,” alisema.
Kuhusu usalama wa maji, alisema Serikali inatarajia kuvifanyia tathmini vyanzo vya maji na jumla ya sampuli 8,000 za maji na sampuli 1,000 za majitaka zitapimwa ili kulinda afya za wananchi na mazingira kwa ujumla.
Alisema wizara yake itaendelea kuimarisha maabara kuu na maabara ya maji ili zipate ithibati na maabara nyingine zitajengewa uwezo kwa kupatiwa wataalamu wa kutosha.
Kambi ya Upinzani
Akiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Sabrina Sungura alisema Serikali imekuwa ikitegemea fedha za wahisani katika kila bajeti.
“Kazi ya kutoa huduma za kijamii duniani kote ni ya Serikali inayokusanya kodi. Kitendo cha Serikali kutegemea mashirika ya nje kugharimia huduma za kijamii kama maji kwa wananchi wetu si sahihi kwa sababu mashirika hayo huchelewesha misaada hiyo au misaada haiji kabisa,” alisema.
Aliitaka Serikali kuondokana na utaratibu wa kutegemea wafadhili kwenye huduma muhimu kama ya maji badala yake, zitengwe fedha za ndani za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata majisafi na salama.
Kuhusu maji vijijini, alisema mradi wa programu za maji vijijini ni dhaifu ikilinganishwa na ule wa mijini wakati vijijini ndiko kwenye mahitaji ya maji kwa ajili ya kilimo.
Sungura alisema takwimu zinaonyesha kuwa mradi wa programu ya maji vijijini kwa mwaka 2011/12 ulitengewa Sh50.8 bilioni wakati programu ya majisafi na majitaka mjini ilitengewa Sh313.55 bilioni.
“Kwa mwaka 2012/13 programu ya maji vijijini imetengewa fedha za ndani Sh9.6 bilioni na fedha za nje Sh27.2 bilioni na programu ya majisafi na majitaka ni Sh126.8 bilioni za ndani na 245.2 bilioni za nje,” alisema.
Alisema Serikali inafanya kosa kubwa la ugawaji wa rasilimali fedha usiozingatia uwiano wa hali halisi ya mahitaji jambo ambalo linaendelea kudidimiza jamii ziishizo vijijini.
Alisema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi vijijini (31,809,808) na ndiyo wenye shida kubwa ya maji ikilinganishwa na wale waishio mijini.
“Tunaitaka Serikali kuanzia bajeti hii kuanza kuangalia ugawaji wa fedha kwa uwiano kati ya programu ya maji vijijini na programu ya majisafi na majitaka mjini ili kuwawezesha wananchi wa vijijini kupata huduma ya maji,” alisema.
Sungura alisema taifa linakabiliwa na uhaba wa wataalamu wa maji kwani wengi waliopo ni wale walisomeshwa miaka ya 1970 na wengi wao wameshastaafu au wanatarajia kustaafu

Chanzo:- Mwananchi
إرسال تعليق