Airtel yatangaza shule 93 za Sekondari Kufaidika na mradi wa Vitabu Airtel shule yetu

Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari ( hawapo pichani) wakati wa hafla maalum ya Mradi na droo ya kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanoyo kama ' AIRTEL SHULEYETU' iliyofanyika katika ofisi za Airtel na kupata shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huo. Kulia  anaefuatilia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi, Hawa Bayumi na Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda (shoto). Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110 
******
Airtel Tanzania, leo imeendeleza dhamira yake katika kuboresha elimu kwa kuchezesha droo iliyochagua shule za sekondari  93 zitakazo faidika na mradi wa vitabu wa Airtel wa kusaidia jamiiunaojulikana kama  Airte shule yetu kwa  mwaka 2012 -2013.

Akiongea katika mkutano na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Airtel Kitengo cha Mawasiliano Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "Mwaka huu, Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia elimu kwa kuzipatia vitabu shule  za sekondari 93, Mradi huu utafaidisha shule 3 kutoka katika kila mkoa Tanzania bara na visiwani.

Shule 93 zilizo chaguliwa leo ni matokeo ya droo iliyochezeshwa na kuzichagua shule hizo kutoka shule 3,000 zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu Tanzania kuwa ni shule ambazo zina uhitaji  mkubwa wa vitabu na kushauri  ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa Airtel shule yetu.

"Toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka saba iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1000 za sekondari zilizopo Tanzania bara na visiwani  kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa  yote  na kuwafikia  wanafunzi katika kila kona ya Tanzania.

Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110, hivyo kila shule  iliyopatikana kwenye droo hii watapata Vitabu alisema Mallya.

 Bi Mallya aliongeza kwa kusema "tumefanya kazi kwa pamoja na Mamlaka ya elimu na Wizara ya Elimu Tanzania kwa kuhakikisha kwamba mahitaji ya vitabu kwa shule zote zitakazoingia kwenye Mradi huu wa Shule yetu tunayatimiza kwa  kuwapatia vitabu vya mitaala ya  masomo yao kama ilivyopendekezwa na Wizara"

"Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwa kutoa misaada mbalimbali ili kuisaidia jamii hapa Tanzania  hasa kwa kuchangia sekta ya elimu kwa kuwapatia vitendea kazi vikiwemo Vitabu  kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Mwaka jana pia Airtel ilisaidia Vitabu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 104 tsh  kwa  shule za sekondari kwa kupitia  droo iliyohusisha jumla ya shule 502" alisema Bi, Mallya.

Nae Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda aliongea kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Ulimu (TEA) alisema "Mamlaka ya Elimu Tanzania tunawashukuru sana.

Airtel kwa dhamira yenu ya kusaidia jamii kwa kuinua kiwango cha elimu hapa nchini " Mradi wa Airtel Shule Yetu ni mradi mzuri sana kwa jamii
yetu kwa kuinua kiwango cha elimu  na maisha ya watanzania"

Tunaamini elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo watanzania wote pamoja na waalimu mtakaopokea vitabu hivi vya mradi wa Airtel Shule yetu tuvitunze na kuvitumia vizuri ili kuunga mkono jitihada za Airtel
katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini" aliongeza kwa kusema Bw, Nyirenda.

Mbali na  shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huu wa vitabu mwaka huu,  pia Airtel Tanzania imeshamaliza kukarabati shule ya msingi ya Kiromo iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kando kando na barabara ya Bagamoyo  ilichaguliwa mwaka jana 2011 huku mipango mingine ya mwaka huu ikiendelea ili kupata shule nyingine itakayofaidika kwa kujengwa na kukarabatiwa na Airtel shule Yetu.

Airtel bado itaendelea kushirikiana wizara ya elimu kwa wadau wengine kuweza kushiriki katika kuinua kiwango cha elimu hapa Tanzania.
 

SCHOOL                              STATUS         DISTRICT            REGION    Year Selected
Karatu+                                  Govt.               Karatu                       Arusha       2012
Loliondo                                 Com                Ngorongoro             Arusha        2012
Kiranyi                                    Com                Arusha (V)                Arusha      2012
Kitomondo                             Com                Mafia                          Pwani         2012
Visiga                                       Com                 Kibaha (M)              Pwani       2012
Changalikwa                          Com                Bagamoyo                  Pwani       2012
Bihawana                                Govt.              Dodoma (V)             Dodoma    2012
Kibakwe                                  Com                Mpwapwa                Dodoma     2012
Pandambili                              Com              Kongwa                    Dodoma      2012
Al-Haramain Sem.               Com            Ilala                              Dar-es-Salaam   2012
Anita's Greenland                 Com            Ilala                            Dar-es-Salaam   2012
Archbishop John sepeku    Com           Ilala                             Dar-es-Salaam   2012
Whitelake                                Com           Kinondoni               Dar-es-Salaam   2012
Mwambao Com     Kinondoni       Dar-es-Salaam   2012
Misitu  Govt.   Kinondoni       Dar-es-Salaam   2012
Yemen   Com     Temeke  Dar-es-Salaam   2012
Hondogo B       Com     Temeke  Dar-es-Salaam   2012
Yeshua  Com     Temeke  Dar-es-Salaam   2012
Itandula        Com     Mufindi Iringa  2012
Furahia (Nee Mnyimau)   Com     Iringa (W)      Iringa  2012
Ukwega  Com     Kilolo  Iringa  2012
Kanyeranyere    Com     Muleba  Kagera  2012
Kirushya        Com     Ngara   Kagera  2012
Nyamigogo       Com     Biharamulo      Kagera  2012
Kumgogo Com     Kibondo Kigoma  2012
Sanuka  Com     Kigoma (V)      Kigoma  2012
Kidahwe Com     Kigoma  Kigoma  2012
Keni    Com     Rombo   Kilimanjaro     2012
Tumo    Com     Hai     Kilimanjaro     2012
Oria    Com     Moshi (V)       Kilimanjaro     2012
Liondo  Com     Nachingwea      Lindi   2012
Namangale       Com     Lindi (V)       Lindi   2012
Kiangara        Com     Liwale  Lindi   2012
Chief Dodo      Com     Babati  Manyara 2012
Ndendo  Com     Kiteto  Manyara 2012
Emboreet        Com     Simanjiro       Manyara 2012
Kukirango       Com     Musoma (V)      Mara    2012
Songe   Com     Musoma (M)      Mara    2012
Kurumwa Com     Tarime  Mara    2012
Mbarali Com     Mbarali Mbeya   2012
Msankwi Com     Mbozi   Mbeya   2012
Imalilo Songwe  Com     Mbarali Mbeya   2012
Matundu Hill (nee Idete)        Com     Kilombero       Morogoro        2012
Malinyi Com     Ulanga  Morogoro        2012
Tushikamane     Com     Morogoro (M)    Morogoro        2012
Lukuledi        Com     Masasi  Mtwara  2012
Nanjota Com     Masasi  Mtwara  2012
Namatutwe       Com     Masasi  Mtwara  2012
Kalebezo        Com     Sengerema       Mwanza  2012
Bugongwa        Com     Mwanza (J)      Mwanza  2012
Kabuhoro        Com     Mwanza (J)      Mwanza  2012
Kabungu Com     Mpanda  Rukwa   2012
Katazi  Com     S'wanga (V)     Rukwa   2012
Korongwe Beach  Com     Nkasi   Rukwa   2012
Nalima  Com     Songea (V)      Ruvuma  2012
Gumbiro Com     Namtumbo        Ruvuma  2012
Luna    Com     Namtumbo        Ruvuma  2012
Kiloleni        Com     Kishapu Shinyanga       2012
Kisuke  Com     Kahama  Shinyanga       2012
Ndala   Com     Shinyanga (M)   Shinyanga       2012
Kimadoi Com     Iramba  Singida 2012
Mitunduruni     Com     Singida (M)     Singida 2012
Mikiwu  Com     Singida (V)     Singida 2012
Bukoko  Com     Igunga  Tabora  2012
Nkiniziwa       Com     Nzega   Tabora  2012
Fundikila       Com     Tabora (M)      Tabora  2012
Magila  Com     Muheza  Tanga   2012
Kwemdimu        Com     Korogwe Tanga   2012
Mkuzi   Com     Lushoto Tanga   2012
Kasamwa Com     Geita   Geita   2012
Nkome   Com     Geita   Geita   2012
Bugalama        Com     Geita   Geita   2012
Yakobi  Com     Njombe  Njombe  2012
Mount Chafukwe  Com     Makete  Njombe  2012
Ikuwo   Com     Makete  Njombe  2012
Somanda Com     Bariadi Simiyu  2012
Old Maswa       Com     Bariadi Simiyu  2012
Mwandete        Com     Maswa   Simiyu  2012
Dodeani Govt.           Pemba South     2012
Kengeja Govt.           Pemba South     2012
Kisiwapanza     Govt.           Pemba South     2012
Wesha   Govt.           Pemba North     2012
Mizingani       Govt.           Pemba North     2012
Makombeni       Govt.           Pemba North     2012
Kidongochekundu Govt.           Unguja Central South    2012
Mpapa   Govt.           Unguja Central South    2012
Ndijani Govt.           Unguja Central South    2012
Mahonda Govt.           Unguja North    2012
High View       Govt.           Unguja North    2012
Mfenesini       Govt.           Unguja North    2012
Fujoni  Govt.           Unguja Urban West       2012
Kitope  Govt.           Unguja Urban West       2012
Matemwe Govt.           Unguja Urban West       2012

Post a Comment

Previous Post Next Post