Santi Cazorla |
Arsenal inajitahidi kukamilisha utiaji saini wa
makubaliano ya mkataba wa kudumu na mchezaji Santi Cazorla kutoka klabu
ya Malaga pamoja na mcheza kiungo mwenzake Nuri Sahin anayeingia kwa
makubalino ya mkopo kutoka klabu ya Real Madrid.
Mpango wa kuhama kwa mchezaji wa Timu ya Taifa
ya Uhispania Cazorla mwenye umri wa miaka 27 kumekua na utata wa shida
ya fedha inayoikumba klabu ya Malaga hata hivyo anatazamiwa kupitia
utaratibu wa afya wiki hii.
Mcheza kiungo wa timu ya Taifa ya Uturuki mwenye
umri wa miaka 23 Nuri Sahin atajiunga na Arsenal chini ya mpango wa
mkopo wa mwaka mmoja na Real Madrid.
Lililobaki ni baina ya mchezaji Sahin
kukubaliana na klabu ya Arsenal juu ya malipo na marupurupu. Kuna
uwezekano mkubwa kwa wachezaji hawa kuhitimisha utaratibu huu kabla ya
msimu mpya kuanza.
Nuri Sahin |
Bado Sahin hajapangiwa siku ya kufanyiwa
majaribio ya afya. Arsenal inaanza msimu mpya kwa pambano la ugenini
dhidi ya Sunderland mnamo tareh 18 Agosti.
Tayari Gunners imewasajili wachezaji wawili
mshambuliaji Lukas Podolski kutoka klabu ya Cologne na mshambuliaji wa
Ufaransa Olivier Giroud aliyekuwa akichezea klabu ya Montpellier.
Pamoja na hayo yote wingu zito bado limegubika
majaliwa ya nahodha Robin van Persie, ambaye ametamka kua hatoongezea
mkataba wake unaomazika mwaka 2013.
Usajili wa wacheza kiungo Cazorla pamoja na
Sahin ingawa hakuna uhusiano na mizengwe ya Van Persie lakini
umechagizwa na habari kwamba mcheza kiungo wa Arsenal Jack Wilshere
hatoweza kucheza kabla ya mwezi oktoba kutokana na jeraha la goti.
Cazorla aliyejiunga na Malaga kutoka klabu ya
Villarreal mwaka mmoja tu uliopita ana urefu wa futi 5 inchi 6 na
ameichezea timu ya Taifa ya Uhispania mwaka 2008 na kwenye mashindano ya
Ulaya ya mwaka 2012.
Sahin alisajiliwa na Real Madrid kutoka Borussia
Dortmund kwa mkataba wa miaka sita mnamo mwezi May 2011 lakini
ameshindwa kupata nafasi katika kikosi Mourinho ambapo kocha huyo
ameweza kumruhusu aondoke tu ila kwa mkopo.
Chanzo:- http://www.bbc.co.uk/swahili/michezo/2012/08/120802_cazorla_sahin.shtml bbc swahili
إرسال تعليق