ARSENAL WAMWAGA VIFAA AIRTEL RISING STAR
![]() |
Mkrugenzi wa Masoko wa Arsenal, Angus Kinnear akimkabidhi jezi, Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga (kushoto) katika sherehe za uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Africa mjini Nairobi leo. |
Nairobi, Kenya
MICHUANO
ya Airtel Rising Stars barani Afrika imetimua vumbi Jijini Nairobi,
Kenya. Michuano hiyo imeleta pamoja wavulana na wasichana wenye umri
chini ya miaka kumi na saba na itaendelea mpaka Agosti 25.
Michuano
hiyo ambayo ilianzia kwenye ngazi ya wilaya mpaka Taifa na kufanyika
kwenye nchi 15 barani Afrika. Huu ni mpango kabambe wa Airtel Rising
Stars, wenye lengo la kuwapa vijana chipukizi fursa ya kuonyesha vipaji
vyao. Ikiwa ni ya moja ya michuano mikubwa kabisa barani Afrika, jumla
ya timu 18,000 zilishiriki na wachezaji 324,000 – wavulana na wasichana
kushiriki. Hii ndio mara ya kwanza kushirikisha wasichana.
Michuano
hiyo ilifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Kenya, Mh Raila Odinga –
akisindikizwa na Mtendaji Mkuu wa Bharti Airtel Afrika – Manoj Kohli
Michuano
hiyo pia itaashiria uzinduzi wa kliniki mbili za soka za kimataifa
zitakaozoendezwa na makocha kutoka klabu kubwa duniani – Arsenal na
Manchester United – zote za Uingereza. Kwenye uzinduzi wa michuano hiyo
pia walikuwa waakilishi kutoka kwenye Klabu hizo – Mkurugenzi wa Masoko
kutoka Manchester United Jonathan Rigby na Mkurugenzi Masoko kutoka
Arsenal Angus Kinnear. Uzinduzi wa kliniki utafanyika na wachezaji wa
zamani wa Manchester United Peter Schmeichel na Ray Parlour kutoka
Arsenal.
Kwenye
mechi za ufunguzi, timu ya wasichana ya Kenya ilishushia kipigo cha
magoli 11 wenzao wa Malawi wakati kwa upande wa wavulana Malawi
ilishinda 5- dhidi ya Kenya
Post a Comment