BALOTELLI ACHA UTOTO DIMBANI - MANCINI

  BALOTELLI ACHA UTOTO DIMBANI - MANCINI

 

Mario Balotelli akiwa na kocha Roberto Mancini


MANCHESTER, England

MTALIANO Roberto Mancini, amemwambia mshambuliaji wake Mario Balotelli kuwa huu ni wakati wa kuanza kuzalisha yaliyo bora kwa klabu yake ya Manchester City.

Wengi walishangazwa na kiwango cha Balotelli katika michuano ya Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2012’ na kuamini kuwa, huo unaweza kuwa mwanzo mpya wa mafanikio katika zama zake za usakataji kabumbu.

Lakini Mancini hataki kushawishika kuwa utata na utukutu kwa nyota huyo umefikia tamati, na kumtaka kuonesha ushahidi wa kimtazamo ndani ya dimba kwa ustawi wa soka lake na mafanikio ya klabu yake.

Mancini alisema: “Mario ni sawa. Labda anaweza kuboresha kiwango, lakini sidhani kama hilo linawezekana kwa mwezi mmoja.

“Kama yeye atacheza kama alivyofanya akiwa katika mashindano ya Euro 2012, basi atakuwa bora mno.

“Lakini yeye ana jukumu kubwa hapa. Kwetu sisi, yeye ni mchezaji muhimu ambaye tulitumia pesa kubwa kumnunua. Yeye anaweza kufanya kazi bora akiwa hapa,” alisisitiza Mancini.

Mtukutu huyu alisajiliwa kwa dau nono la pauni milioni 22 akitokea Inter Milan ya Italia miaka miwili iliyopita, ambapo maisha ya utata ndani na nje ya uwanja yametia shakani kipaji chake.

Post a Comment

أحدث أقدم