HAYA NI BAADHI YA MAGAZETI YA ULAYA LEO - MICHEZO

CHELSEA KUSAINI BEKI LA NGUVU LA HISPANIA

Yann M'Vila is the subject of bids from Tottenham, Zenit St Petersburg and an unnamed club.Beki wa kulia wa Marseille, Cesar Azpilicueta amesema amekuwa akifuatiliwa na Chelsea ili akachukue mikoba Jose Bosingwa. Azpilicueta, aliyezaliwa miaka 22 iliyopita, alikuwemo kwenye kikosi cha Hispania kilichoshiriki Michezo ya Olimpiki mjini London mwaka huu.

Liverpool inaona bora mshambuliaji wake, Andy Carroll mwenye umri wa miaka 23 akae benchi msimu mzima, kuliko kumuuza kwa bei ya chini kwa wapinzani wao katika Ligi Kuu.

Newcastle na Fulham zinamfuatilia beki wa FC Twente, Douglas. Mzaliwa huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 anacheza chini ya kocha wa zamani wa England, Steve McLaren katika Ligi Kuu ya Uholanzi.


Rennes ya Ufaransa, inatarajia kiungo wake kinda, Yann M'Vila, mwenye umri wa miaka 21, ataondoka kwenye klabu hiyo wiki hii. Timu hiyo ya Ligue 1 imesema imepokea ofa Tottenham, Zenit St Petersburg na klabu nyingine ya tatu ambayo hawakuitaja, ambayo hata hivyo inaaminika kuwa ni Arsenal.

Newcastle iliyoonyesha nia ya kumrudisha Carroll, imesema hataongeza dau kutoka pauni Milioni 12 walizoahidi kwa ajili ya mchezaji huyo, ambaye The Magpies walimuuza kwa Wekundu wa Anfield pauni Milioni 35, Januari mwaka jana.

Post a Comment

Previous Post Next Post