CHELSEA KUSAINI BEKI LA NGUVU LA HISPANIA
![Yann M'Vila is the subject of bids from Tottenham, Zenit St Petersburg and an unnamed club.](http://news.bbcimg.co.uk/media/images/62416000/jpg/_62416881_m%27vila_getty.jpg)
Liverpool inaona bora mshambuliaji wake, Andy Carroll mwenye
umri wa miaka 23 akae benchi msimu mzima, kuliko kumuuza kwa bei ya
chini kwa wapinzani wao katika Ligi Kuu.
Newcastle na Fulham zinamfuatilia beki wa FC Twente, Douglas.
Mzaliwa huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 anacheza chini ya kocha
wa zamani wa England, Steve McLaren katika Ligi Kuu ya Uholanzi.
Rennes ya Ufaransa, inatarajia kiungo wake kinda, Yann M'Vila,
mwenye umri wa miaka 21, ataondoka kwenye klabu hiyo wiki hii. Timu hiyo
ya Ligue 1 imesema imepokea ofa Tottenham, Zenit St Petersburg na klabu
nyingine ya tatu ambayo hawakuitaja, ambayo hata hivyo inaaminika kuwa
ni Arsenal.
Newcastle iliyoonyesha nia ya kumrudisha Carroll, imesema hataongeza dau
kutoka pauni Milioni 12 walizoahidi kwa ajili ya mchezaji huyo, ambaye
The Magpies walimuuza kwa Wekundu wa Anfield pauni Milioni 35, Januari
mwaka jana.
إرسال تعليق