HII NDIYO SIRI YA SIMBA KUWEKA KAMBI ARUSHA

HII NDIYO SIRI YA SIMBA KUWEKA KAMBI ARUSHA

Kikosi cha Simba SC

Na Princess Asia
KLABU ya Simba imesema kwamba, imeweka kambi Arusha kwa sababu mbili kubwa,
1.  Wanaona wana bahati na mkoa huo na 
2.  Ni sehemu nzuri kwa mazoezi kutokana na hali yake ya hewa.
Ofisa Habari wa mabingwa hao wa Ligi Kuu, Ezekiel Kamwaga alisema jana kwamba Arusha ni mkoa ambao una hali ya hewa ya baridi, hivyo wachezaji wanafanya mazoezi kwa muda mrefu bila kuchoka.
“Kwa hiyo wakitoka huko na kurudi Dar es Salaam, wataweza kucheza vizuri sana wakiwa fiti kiasi cha kutosha kutokana na mazoezi mengi ya Arusha,”alisema.
Aidha, Kamwaga alisema kwamba msimu uliopita Simba iliweka kambi Arusha pia na ikafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kuwafunga wapinzani wao wa jadi, Yanga SC mabao 5-0.
“Kwa hiyo mambo hayo mawili makubwa ndio yalitufanya tuweke tena kambi Arusha na tunaamini kabisa tutanga’ara kama msimu uliopita,”alisema.
Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi mjini Arusha kwa wiki mbili sasa chini ya kocha wake Mkuu, Mserbia Profesa Milovan Cirkovick na kitaanza msimu mpya kwa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya washindi wa pili wa ligi hiyo, Azam FC

Post a Comment

Previous Post Next Post