HII NDIYO SIRI YA SIMBA KUWEKA KAMBI ARUSHA
Kikosi cha Simba SC |
Na Princess Asia
KLABU
ya Simba imesema kwamba, imeweka kambi Arusha kwa sababu mbili kubwa,
1. Wanaona wana bahati na mkoa huo na
2. Ni sehemu nzuri kwa mazoezi
kutokana na hali yake ya hewa.
Ofisa
Habari wa mabingwa hao wa Ligi Kuu, Ezekiel Kamwaga alisema jana kwamba
Arusha ni mkoa ambao una hali ya hewa ya baridi, hivyo wachezaji
wanafanya mazoezi kwa muda mrefu bila kuchoka.
“Kwa
hiyo wakitoka huko na kurudi Dar es Salaam, wataweza kucheza vizuri
sana wakiwa fiti kiasi cha kutosha kutokana na mazoezi mengi ya
Arusha,”alisema.
Aidha,
Kamwaga alisema kwamba msimu uliopita Simba iliweka kambi Arusha pia na
ikafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kuwafunga wapinzani
wao wa jadi, Yanga SC mabao 5-0.
“Kwa
hiyo mambo hayo mawili makubwa ndio yalitufanya tuweke tena kambi
Arusha na tunaamini kabisa tutanga’ara kama msimu uliopita,”alisema.
Kikosi
cha Simba kinaendelea na mazoezi mjini Arusha kwa wiki mbili sasa chini
ya kocha wake Mkuu, Mserbia Profesa Milovan Cirkovick na kitaanza msimu
mpya kwa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya washindi wa pili wa ligi hiyo,
Azam FC
إرسال تعليق