NURI SAHIN AAMUA KUTUA ARSENAL, AKATAA KUPELEKWA LIVERPOOL FC
Kiungo wa Real Madrid, Nuri Sahin, mwenye umri wa miaka 23,
ametaka mpango wa kupelekwa kwa mkopo Liverpool usitishwe na badala yake
apelekwe Arsenal, ambayo nyota huyo wa zamani wa Dortmund anatumaini
itamsaidia kung'ara kutokana na kucheza Ligi ya Mabingwa.
Fulham imefufua nia yake ya kumsajili kiungo wa Blackburn, Steven
N'Zonzi, mwenye umri wa miaka 23, ambaye hayuko kwenye mipango ya Steve
Kean, baada ya kugoma kuichezea klabu hiyo msimu uliopita.
Liverpool inataka kumsajli ama mmoja kati ya wachezaji wawili wa Spurs
Steven Caulker au Michael Dawson, ikiwa beki Daniel Agger atahamia
Manchester City.
Mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas Bendtner amesistiza msimamo
wake wa kutaka kuihama klabu hiyo, akisema kwamba hatakuwa na furaha
hadi afanye hivyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, msimu uliopita
alicheza kwa mkopo Sunderland, lakini hajafanikiwa kuhamishwa moja kwa
moja.
Mabingwa wa Urusi, Zenit St Petersburg wana nia ya kumsajili
mshambuliaji wa Manchester United, Dimitar Berbatov. Mshambuliaji huyo
mwenye umri wa miaka 31 wa Bulgaria, amekwishaambiwa anaweza kuondoka
Old Trafford.
إرسال تعليق