YANGA YAZURU MAKABURI YA WAHANGA WA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA
![]() |
Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa klabu ya Young Africans, Mama Fatma Karume akiwaongoza viongozi na wachezaji wa yanga kwenda kuweka mashada ya maua katika makaburi ya mauaji ya Kimbari katika eneo la gisozi jijini kigali |
Timu ya Young Africans iliyoko Kigali nchini Rwanda imetembelea eneo la makumbusho ya mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 na kusababisha wanyarwanda wengi kupoteza maisha katika vita iliyohusisha makabila mawili tofauti.
Young Africans iliyoko nchini Rwanda kwa ziara ya mafunzo ya wiki moja, jana jioni ilifanya mazoezi katika uwanja wa Nyamahoro kujiandaa na mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports, mchezo utakaochezwa hapo kesho majira ya jioni.
![viongozi wa yanga wakisubiri kuzuru na kuweka mashada ya maua katika makaburi ya mauaji ya kimbari mwaka 1994.](http://www.youngafricans.co.tz/images/stories/a3.jpg)
![Young Africans wakiwasili katika makaburi ya mauaji ya kimbari mjini kigali](http://www.youngafricans.co.tz/images/stories/a2.jpg)
![Wachezaji na Viongozi wa yanga wakipata maelezo kabla ya kuingia kutembelea nyumba ya makumbusho ya mauaji ya kimbari](http://www.youngafricans.co.tz/images/stories/a4.jpg)
![Jeryson Tegete akimtoka Godfrey Taita, wakati wa mazoezi katika uwanja wa Nyamirambo](http://www.youngafricans.co.tz/images/stories/a5.jpg)
![Saimon Msuva (kulia) akichuana na Jeryson Tegete (kushoto) wakati wa mazoezi](http://www.youngafricans.co.tz/images/stories/a6.jpg)
![Wachezaji wa Young Africans wakiwa wamejipumzisha katika hoteli ya kisasa ya La pallais mjini kigali (picha zote na Saleh Ally)](http://www.youngafricans.co.tz/images/stories/a7.jpg)
إرسال تعليق