Inter yapata wamiliki wa bara Asia

Klabu ya Uitaliano Inter Milan inasema kua kundi la wawekezaji kutoka Uchina limejitokeza kua wawekezaji wa pili kwa ukubwa wa kumiliki hisa za klabu hiyo.
Katika taarifa ya Internazionale Holding,kampuni mama inayosimamia masuala yote yanayohusiana na klabu imesema kua kundi hilo limetangaza kua litamiliki sehemu ya hisa lakini kwamba familia ya Moratti itaendelea kumiliki sehmu kubwa ya biashara.
Taarifa hio imesema kua uwanja mpya utajengwa chini ya ushirikiano na sehemu ya China Railway Construction ikitazamiwa kukamilishwa mnamo mwaka 2017.
Klabu hio imetangaza kua Kamchi Li, Kenneth Huang na Fabrizio Rindi wote watakua wakurugenzi kwenye bodi kutokana na uwekezaji huu.
Inter ndio klabu ya hivi karubini kuvutia wawekezaji kutoka barani Asia. Klabu ya jijini London na Ligi kuu ya Premiership Queen's Park Rangers ina milikiwa na Tony Fernandes, huyu akiwa mmiliki wa kampuni uya ndege baranoi Asia, Air Asia, baada ya kukamilisha ununuzi wake mwaka jana.

Post a Comment

Previous Post Next Post