Michel Morganella |
Timu ya mpira wa miguu ya Uswizi imemfukuza beki wake
Michel Morganella kutoka mashindanoni kwa kutuma ujumbe wa ki-ubaguzi
wa rangi akitumia mtandao wa Twitter.
Mchezaji huyo alituma ujumbe ukiwalenga watu wa
Korea ya kusini kwa ujumla kupitia Twitter baada ya Timu yake kupoteza
mechi dhidi ya Korea ya kusini 2-1 jumapili iliyopita.
Tangu
hapo mtandao huo umefutwa na beki huyo kuomba radhi, akisema kweli,
nilikosea sana baada ya matokeo yasiyoridhisha, alisema kijana huyo
mwenye umri wa miaka 23.
Morganella aliongezea kusema kua: "ningependa
kuwaomba radhi raia wote wa Korea ya kusini na timu yao, vilevile ujumbe
wa Uswizi na mchezo wa mpira kwa ujumla nchini Uswizi."
Mapema mwezi huu, mwanariadha wa Ugiriki wa
kuruka hatua tatu kuelekea mchangani Paraskevi Papachristou alitimuliwa
kutoka kwenye kikosi cha Olimpiki cha nchi yake kufuatia matamshi
aliyoyatoa kupitia Twitter yaliyoonekana kuwa ya kiubaguzi wa rangi.
Kocha mkuu wa Kikosi cha Uswizi Gian Gilli
alisema kua Morganella, anayecheza soka yake ya kulipwa na klabu ya
Italia -Palermo ameidhalilisha timu nzima. Kocha huyo amesema kua
alibagua, katukana na kukiuka hadhi ya raia na wachezaji wa timu nzima
ya Korea ya kusini.
Habari na bbc swahili
Post a Comment