Arsenal kusajili wawili kwa mpigo

Santi Cazorla
Arsenal inajitahidi kukamilisha utiaji saini wa makubaliano ya mkataba wa kudumu na mchezaji Santi Cazorla kutoka klabu ya Malaga pamoja na mcheza kiungo mwenzake Nuri Sahin anayeingia kwa makubalino ya mkopo kutoka klabu ya Real Madrid.
Mpango wa kuhama kwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uhispania Cazorla mwenye umri wa miaka 27 kumekua na utata wa shida ya fedha inayoikumba klabu ya Malaga hata hivyo anatazamiwa kupitia utaratibu wa afya wiki hii.
Mcheza kiungo wa timu ya Taifa ya Uturuki mwenye umri wa miaka 23 Nuri Sahin atajiunga na Arsenal chini ya mpango wa mkopo wa mwaka mmoja na Real Madrid.
Lililobaki ni baina ya mchezaji Sahin kukubaliana na klabu ya Arsenal juu ya malipo na marupurupu. Kuna uwezekano mkubwa kwa wachezaji hawa kuhitimisha utaratibu huu kabla ya msimu mpya kuanza.

Nuri Sahin
Bado Sahin hajapangiwa siku ya kufanyiwa majaribio ya afya. Arsenal inaanza msimu mpya kwa pambano la ugenini dhidi ya Sunderland mnamo tareh 18 Agosti.
Tayari Gunners imewasajili wachezaji wawili mshambuliaji Lukas Podolski kutoka klabu ya Cologne na mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud aliyekuwa akichezea klabu ya Montpellier.
Pamoja na hayo yote wingu zito bado limegubika majaliwa ya nahodha Robin van Persie, ambaye ametamka kua hatoongezea mkataba wake unaomazika mwaka 2013.
Usajili wa wacheza kiungo Cazorla pamoja na Sahin ingawa hakuna uhusiano na mizengwe ya Van Persie lakini umechagizwa na habari kwamba mcheza kiungo wa Arsenal Jack Wilshere hatoweza kucheza kabla ya mwezi oktoba kutokana na jeraha la goti.
Cazorla aliyejiunga na Malaga kutoka klabu ya Villarreal mwaka mmoja tu uliopita ana urefu wa futi 5 inchi 6 na ameichezea timu ya Taifa ya Uhispania mwaka 2008 na kwenye mashindano ya Ulaya ya mwaka 2012.
Sahin alisajiliwa na Real Madrid kutoka Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka sita mnamo mwezi May 2011 lakini ameshindwa kupata nafasi katika kikosi Mourinho ambapo kocha huyo ameweza kumruhusu aondoke tu ila kwa mkopo.
Chanzo:- http://www.bbc.co.uk/swahili/michezo/2012/08/120802_cazorla_sahin.shtml bbc swahili

Post a Comment

Previous Post Next Post