KADI NYEKUNDU HEWA ALIYOPEWA IVANOVIC KUTOFUNGIWA HATA MECHI MOJA
BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic
hatapewa adhabu yoyote ya kukosa mechi licha ya kutolewa nje kwa kadi
nyekundu jana katika mechi ya Ngao ya Jamii waliyofungwa na Man City.
Mserbia huyo alitolewa nje mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kumchezea rafu mwananchi mwenzake, Aleksandar Kolarov na
refa Kevin Friend akamlimla nyekudu ya papo kwa papo.
Iliripotiwa kwamba Ivanovic atafungiwa
mechi tatu, kuanzia mechi ya ufunguzi ya Chelsea ya Ligi Kuu ya England
dhidi ya Wigan Jumapili ijayo, pamoja na hayo mabadiliko ya sheria za FA
Agosti mwaka 2009, yanayosema kadi nyekundu katika mechi za kujiandaa
na msimu mpya haitamzuia mchezaji kucheza mechi za mashindano ndio
yanamnusuru.
Kwa mabadiliko hayo ya sheria yanayohusu mechi zote zisizo za mashindano za kujiandaa na msimu mpya,
ikiwemo mechi ya Community Shield, inamaanisha Ivanovic atakuwa huru kucheza Uwanja wa DW.
RAFU YENYEWE: Kolarov akiangushwa chini na Ivanovic
Imwtafsiliwa na http://bongostaz.blogspot.com/ Kwa hisani ya
إرسال تعليق