KENYA HALI SASA SHWARI BAADA YA GHASIA ZA SIKU TATU

KENYA HALI SASA SHWARI BAADA YA GHASIA ZA SIKU TATU

Mji wa Mombasa ulikuwa na vurugu baada ya kifo cha Sheik Aboud Rogo
Hali Mjini wa Mombasa nchini Kenya inasemekana kuwa shwari kufuatia ghasia zilizoanza siku ya jumatatu baada ya kuuwawa kwa kiongozi wa kidini anayehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab sheikh Aboud Rogo Mohammed.
Tangu kuuwawa kwa kiongozi huyo kumekuwa na ghasia za hapa na pale mjini Mombasa, Tayari watu 24 wamefikishwa mahakamani kufuatia ghasia hizo. Kwa sasa serikali imeunda jopo la watu 11 kuchunguza mauaji ya Sheikh Rogo na pia ghasia zilizosababisha mauaji ya watu wanne wakiwemo maafisa watatu wa polisi.
Amina Abubakar amezungumza na mwandishi wetu wa Mombasa Eric Ponda juu ya hali halisi ya mambo kwa sasa

Sikiliza mazungumzo kati ya Amina Abubakar na Eric Ponda bofya hapa


Mwandishi Amina Abubakar
Chanzo:- DW Swahili

Post a Comment

أحدث أقدم