KIPA
wa kwanza wa timu ya taifa ya Somalia chini ya umri wa miaka
17, Abdulkader Dheere Hussein ameuawa mjini Mogadishu na watu
wasiojulikana, Shirikisho la Soka Somalia (SFF) limesema.
Kipa
huyo kijana, aliuawa katika Wilaya ya Waberi mjini Mogadishu, baada ya
kutokea mazoezini. “Bado hatujui nani alikuwa nyuma ya mauaji haya,
lakini shirikisho la soka Somalia inafanyia uchunguzi suala hilo, ili
kujua nani haswa alihusika na mauaji huyo.
Katibu Mkuu wa SFF, Jenerali Abdi Qani Said Arab amesema katika taarifa yake ya Julai 26.
Rais
wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou amesikitishwa na
mauaji hayo na kutoa salamu za pole kwa familia ya marehemu na wapenzi
wa soka Somalia. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amiin.
Post a Comment