PAUNI MILIONI 30 ZA MAN CITY KUMTAKA DAVID LUIZ - CHELSEA WAZITOLEA NJE.
![Jesus Navas](http://news.bbcimg.co.uk/media/images/62438000/jpg/_62438429_jesusnavas_getty.jpg)
Mmiliki wa Liverpool, John W Henry yuko tayari kuuzwa kwa viungo
Charlie Adam na Jay Spearing -ili kutafuta fedha za kumnunua nyota wa
Fulham, Mmarekani Clint Dempsey.
Habari kamili: Daily Mirror
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema yuko tayari kumtoa
kwa mkopo kiungo wa kimataifa wa Uturuki, Nuri Sahin katika klabu ya
England, lakini hawezi kujali kama atakwenda Arsenal, Liverpool au
Tottenham.
Habari kamili: Guardian![Robert Lewandowski](http://news.bbcimg.co.uk/media/images/62438000/jpg/_62438427_robertlewandowski_getty.jpg)
Klabu mbili za Milan, Inter na AC, zinagombea saini ya thamani ya pauni
Milioni 8 ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi,Nigel de Jong, mwenye
umri wa miaka 27, kutoka Manchester City. De Jong, ambaye alijiunga na
City akitokea Hamburg kwa pauni Milioni 18, Januari 2009, amebakiza
mwaka mmoja tu katika mkataba wake Manchester na anaweza kuondoka.
Habari kamili: Goal.com
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Eduardo, mwenye umri wa miaka
29, amesema hakuwahi kujua kama alikuwa anatakiwa na Fulham kwa pauni
Milioni 7, lakini amesema ni bora aondoke klabu yake ya sasa, Shakhtar
Donetsk na kujiunga na klabu yoyote ya Ligi Kuu ya England.
Habari kamili: Independent
Post a Comment