PAUNI MILIONI 30 ZA MAN CITY KUMTAKA DAVID LUIZ - CHELSEA WAZITOLEA NJE.
Chelsea imekataa ofa ya pauni Milioni 30 kutoka Manchester City
kutaka kumnunua beki wao, wa Kibrazil, David Luiz mwenye umri wa miaka
30. City inakabiliwa na tatizo la beki, na Micah Richards anatakiwa kuwa
nje kwa wiki 10 kwa sababu ya majeruhi.
Mmiliki wa Liverpool, John W Henry yuko tayari kuuzwa kwa viungo
Charlie Adam na Jay Spearing -ili kutafuta fedha za kumnunua nyota wa
Fulham, Mmarekani Clint Dempsey.
Habari kamili: Daily Mirror
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema yuko tayari kumtoa
kwa mkopo kiungo wa kimataifa wa Uturuki, Nuri Sahin katika klabu ya
England, lakini hawezi kujali kama atakwenda Arsenal, Liverpool au
Tottenham.
Habari kamili: Guardian
Theo Walcott akiwa
amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake, Arsenal inajipanga kwa
lolote kwa kutaka kumsajili nyota wa Sevilla, Jesus Navas. Mchezaji wa
kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 26 anaweza kuuzwa kwa pauni
Milioni 35, lakini klabu yake inaweza kupokea fedha chini ya kiwango
hicho.
Klabu mbili za Milan, Inter na AC, zinagombea saini ya thamani ya pauni
Milioni 8 ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi,Nigel de Jong, mwenye
umri wa miaka 27, kutoka Manchester City. De Jong, ambaye alijiunga na
City akitokea Hamburg kwa pauni Milioni 18, Januari 2009, amebakiza
mwaka mmoja tu katika mkataba wake Manchester na anaweza kuondoka.
Habari kamili: Goal.com
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Eduardo, mwenye umri wa miaka
29, amesema hakuwahi kujua kama alikuwa anatakiwa na Fulham kwa pauni
Milioni 7, lakini amesema ni bora aondoke klabu yake ya sasa, Shakhtar
Donetsk na kujiunga na klabu yoyote ya Ligi Kuu ya England.
Habari kamili: Independent
إرسال تعليق