MBUNIFU WA MAVAZI ALLY REHMTULLAH MITINDO MIPYA YA MAVAZI MWEZI UJAO.

Na Mwandishi Wetu.
Mwanamitindo maarufu nchini Ally Rehmtullah ameandaa onyesho kubwa na la kipekee la mitindo hapa nchini litakalofanyika tarehe 8 Mwezi ujao katika jiji la Dar es Salaam na kuonyeshwa moja kwa moja katika mtandao wa www.ar.co.tz ambapo pia atazindua rasmi kazi zake mpya za mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanaume na wanawake.

Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Rehmtullah amesema dhumuni la kuandaa onyesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha aina mpya ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati zake za kuinua kiwango cha kazi za mitindo ndani ya nchi.

Mesema amepanga kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini ili kazi za wanamtindo na wabunifu wa mavazi ziweze kupenya kwenye soko la ndani na la Afrika mashariki na kati wakati tayari kuna soko la pamoja katika jumuiya ya Afrika mashariki.

Rehmtullah amesema kwamba onyesho hilo litakuwa la kipekee kwa sababu mavazi na onyesho litapambwa na rangi nyeupe, ubunifu wa hali ya juu pamoja na muonekano mpya wa mavazi yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza kuendana na utamaduni wa mwafrika.

Amesema onyesho hilo litakalofanyika katika hoteli ya Serena litapambwa na wasanii mbalimbali wa muziki na wacheza shoo kutoka sehemu mbalimbali.

Rehmtullah amesema onyesho hilo itakuwa ni nafasi ya kipekee kwa yeye binafsi kuonyesha muonekano mpya wa tasnia ya mitindo hapa nchini na nje ya nchi ili kuonyesha ni kwa jinsi gani wanamitindo wa kitanzania wanavyoweza kuonyesha kazi zao.

Ameongeza kuwa tasnia ya mitindo kwa ujumla ina nafasi ya kipekee kwa wanamtindo chipukizi kujitokeza na kuonyesha kazi zao kwa watu mbalimbali hasa washika dau katika sekta hiyo.

Onyesho hilo linategemewa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 400 wakiwemo viongozi mbalimbali kama mawaziri, wabunge, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mashirika mbalimbali.

Onyesho hilo litakuwa ni la mialiko maalum na limepewa jina la Ally Rehmtullah 2013 collection.

Wadhamini wa onyesho hilo ni Mercedez Benz, Belvedere Vodka, DULUX, RAHA, HUGO DOMINGO,THE Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm Plant, Creative Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia Properties, Dar es Salaam Serena Hotel, Missie Popular Blog, MO BLOG,Quality Furniture na Mx Carter.

Post a Comment

أحدث أقدم