Mshambuliaji
wa kimataifa kutoka timu ya Olympic Atletico ya Burundi, Didier
Kavumbagu amewasili jana usiku na kujiunga na kikosi cha mabingwa wa
Afrika Mashariki na Kati Young Africans Sports Club tayari kwa kuanza
kuitumikia timu yake mpya.
Didier Kavumbagu aliyechezea
timu ya Olympic Atletico katika mashindano ya Kagame ya mwaka huu na
kuifikisha timu yake hatua ya Robo Fainali, kabla ya kutolewa na timu ya
URA ya Uganda.
Pamoja na timu yake kutolewa katika hatua ya robo
fainali, Didier aionyesha kiwango cha hali ya juu ikiwa ni pamoja
kufunga mabao yote mawili katika mchezo wa kwanza wa Ufunguzi wa
mashindano ya Kagame dhidi ya Young Africans.
Mchezaji huyu wa
timu ya Taifa ya Burundi amesajliwa kuichezea timu ya Young Africans
kwa mkataba wa miaka miwili ambapo atakua mitaa ya twiga na jangwani
mapaka mwishoni mwa msimu wa 2013-2014.
Kavambagu alizaliwa tarehe
02/05/1988 mjini Bujumbura na kuanza kucheza soka katika timu za
mitaani kabla ya kuchaguliwa timu ya taifa ya vijana U-17 mwaka 2006 na
kushiriki mashindano ya kombe la vijana CECAFA U-17 visiwani Zanzibar.
Alionyesha
kiwango cha hali ya juu katika mashindano hayo na kupelekea kusajiliwa
na timu ya Olympic Atletico ambapo ameitumikia mpaka mwaka huu alipoamua
kuachana na yo na kujiunga na mabingwa wapya wa kombe la Kagame Young
Africans Sports Club.
Young Africans imeanza jana mazoezi yake kwa
ajiliya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaotazamiwa
kuanza septemba mosi, na wachezaji wote wamehudhuria mazoezi jana na leo
Didier amejumuika na wachezaji wenzake kufanya mazoezi chini ya kocha
Mkuu Tom Saintfiet katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola.
Post a Comment