NEWS; NGASSA ATUA SIMBA KWA MILIONI 25
Ngassa sasa wa Simba |
MRISHO Khalfan Ngassa ameuzwa Simba kwa dau la Sh. Milioni
25 mchana wa leo, Azam imethibitisha.
Habari za ndani kutoka Azam, zimesema kwamba Simba wamelipa
fedha hizo na wamesainiwa fomu za uhamisho na sasa Mrisho anafuata nyayo za
baba yake Khalfan Ngassa, ambaye aliichezea Simba SC 1991/1992.
Azam ilifikia uamuzi wa kumuuza Ngassa, baada ya
mchezaji huyo iliyesajiliwa kutoka Yanga miaka miwili iliyopita, kubusu jezi ya
Yanga baada ya kufunga bao la pili katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC),uamuzi huo, ni wa mzee Said Salim Bakhresa
mwenyewe, ambaye alikerwa na kitendo hicho akawaagiza wanawe, Wakurugenzi wa
bodi ya timu wamuuze mchezaji huyo popote, haraka iwezekanavyo.
إرسال تعليق