
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania Dioniz Malinzi akikata utepe kuzindua
tamasha la Rock City Marathon 2012, katika hafla iliofanyika jana katika
hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Picha na Mwandishi wetu

Wadhamini
wa tamasha la Rock City Marathon 2012, pamoja na Mwenyekiti wa Baraza
la Michezo Tanzania Dioniz Malinzi (wa tatu kulia) wakiwa katika picha
ya pamoja katika hafla ya uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika jana
katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
********
MWENYEKITI
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi, amezindua toleo
la nne mbio za Rock City Marathon, zitakazofanyika kuanzia Oktoba 28
mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Akizungumza
katika uzinduzi huo jana kwenye hoteli ya New Africa, Dar es Salaam,
Malinzi alisema ni wakati wa kukufua vipaji vya mchezo wa riadha
nchini.
“Kwanza
nawashukuru Kampuni ya Capital Plus Internationa kwa kuendelea kuandaa
mbio hizi kwa miaka mine sasa, sio siri michezo Tanzania imedorora,
kwani tumechukua dhamana ya michezo lakini baadhi ya watu wamekua
walafi, wanajenga majumba Mbezi Beach na kuendesha magari ya kifahari.
“Hii
yote imechangiwa na dhamana ya uongozi wa michezo kuwapa walafi ambao
wametufikisha hapa, nawaomba Capital Plus International msiishie hapa,
tunataka sasa tufufue vipaji vya riadha na mwaka huu tumeamua tuwe na
mashindano ya Taifa ya Riadha,” alisema Malinzi.
Tukio
hilo limewavutia wadau wengi michezo, pamoja na makampuni makubwa kama
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB), African Barrick Gold, Nyanza Bottlers, Mfuko wa Pensions (PPF),
Geita Gold Mine, TANAPA, Sahara Communication, ATCL, New Mwanza Hotel,
Airtel, na New Africa Hotel ambao wamejitokeza kudhamini mbio hizo.
Alisema
mbio za mwaka huu zitahusisha mashindano mbalimbali kama vile mbio za
nyika kilomita 5, (ambazo sio za ushindani), bali zitafanyika kama moja
ya maandalizi ya mbio za mfano wa Marathon (mini marathon), pia
kutakuwa na mbio za nusu Marathon za kilomita 21, mbio za kujifurahisha
maarufu kama Fun Race (Classic for all) kilomita 5, mbio za walemavu
za kilomita 3, mbio za watu wazima za kilomita 3 na mbio za watoto
kuanzia miaka saba hadi 10 zenye urefu wa kilomita 2.
Kwa
upande wake Msemaji wa Capital Plus International, Dk. Ellen Otaru,
alisema mbio hizo zinaenda sambamba na kuhamasisha Utalii wa ndani
kupitia sekta ya michezo, ambapo washiriki watakua ni kutoka Ziwa
Victoria na nchi jirani kama Kenya, Uganda, Afrika Kusini na baadhi ya
Mataifa ya Ulaya.
“Ningependa
kutoa shukrani kwa wafadhili mbalimbali waliofanikisha mashindano
haya, nasi Capital Plus International, tunataka kuwahakikishia kuwa
tunakuza riadha nchini na kuleta medali za dhahabu,” alisema.
Kwa
upande wake, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Riadha Tanzania (RT), William
Kalage, alisema wameridhia uwezo wa Capital Plus International katika
kuandaa mbio hizo
Post a Comment