SAMATTA APIGA LA 4 KLABU BINGWA AFRIKA, MGHANA CLOTTEY KINARA WA MABAO, ABOUTRIKA, MPUTU No.2
Straika Samatta akifanya vitu vyake jana kabla kutupia goli 'kali' la kichwa. |
Straika Samatta akiokota mpira wavuni baada ya kuifungia Mazembe katika mechi mojawapo ya Klabu Bingwa Afrika. |
LUBUMBASHI,
Kongo
Mbwana Samatta
amepanda hadi katika nafasi ya tatu ya wakali wanaoongoza kwa kupachika mabao
katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kupiga goli kali la kichwa na kuisaidia
klabu yake ya TP Mazembe ya Kongo kuibuka na ushindi ‘mtamu’ wa mabao 2-0 dhidi
ya Zamalek ya Misri katika mechi yao ya Kundi B iliyochezwa jana mjini
Lubumbashi.
Hadi mapumziko,
timu hizo zilikuwa hazijafungana. Kiungo Ngandu Kasongo aliifungia Mazembe bao
la utangulizi katika dakika ya 70.
Wenyeji
walipata
bao la pili dakika saba baadaye wakati straika wa kimataifa wa
Tanzania,
Mbwana Samata alipowazidi ujanja mabeki wa Zamalek kwa kuruka juu peke
yake kuuwahi mpira wa 'fri-kiki' kutoka kushoto mwa uwanja na kufunga
bao safi la kichwa lililokuwa la nne kwake katika michuano hiyo msimu
huu.
Maelfu ya
mashabiki waliojazana kwenye uwanja mpya wa Mazembe mjini Lubumbashi unaoingiza
watu 15,000 walilipuka kwa shangwe kutokana na bao la Samatta lililowapa matumaini
ya kupata pointi zote tatu.
Ushindi huo
uliipaisha Mazembe hadi katika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi lao la B kufuatia
wapinzani wao katika kuwania nafasi hiyo, klabu ya Berekum Chelsea ya Ghana, kukubali
kipigo kizito cha ugenini cha mabao 4-1 kutoka kwa vinara Al Ahly.
Katika msimamo,
Al Ahly wanaongoza wakiwa na pointi tisa baada ya kushinda katika mechi zote
tatu na kufuatiwa na Mazembe wenye pointi nne, sawa na Chelsea lakini Waghana
wakizidiwa na akina Samatta kwa tofauti ya mabao.
Kipigo
kutoka kwa Mazembe kilizidi kuichimbia mkiani klabu ya Zamalek isiyokuwa na
pointi baada ya kufungwa katika mechi zote, na ambayo kabla ya mechi hiyo iliachana
na kocha Hassan Shehata aliyeamua kubwaga manyanga kutokana na mfululizo wa
matokeo mabaya.
Ushindi pia
umeongeza matumaini ya Mazembe kutinga nusu fainali kwani timu mbili za kundi
lao la B na nyingine za idadi hiyo kutoka Kundi A ndizo zitakazosonga mbele kwa
hatua inayofuata.
Baada ya bao
lake la nne jana, Samatta amepanda katika orodha ya majina ya wanaoongoza kwa ufungaji
na kushika nafasi ya tatu, akitanguliwa na Mghana Emmanuel Clottey wa Berekum
Chelsea aliyeongeza bao jingine jana wakati timu yake ikilala 4-1 na hivyo
kufikisha mabao 12 huku Mohamed Aboutrika wa Ahly na Tressor Mputu (TP Mazembe)
wakikamata nafasi ya pili baada ya kila mmoja kufikisha magoli sita.
Clottey
amebakiza bao moja kufikia rekodi ya mabao katika historia ya michuano hiyo iliyowekwa
msimu wa 2007 na Mnigeria Stephen Worghu.
Orodha ya
wakali wa mabao katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika baada ya mechi za jana:
12 Emmanuel
Clottey (Berekum Chelsea)
6 Tresor Mputu (TP Mazembe)
Mohamed Aboutrika (Al-Ahly)
4 Mbwana Samatta (TP Mazembe)
Karim Ali Hadji (ASO Chlef)
Rasca (Recreativo do Libolo)
Izu
Azuka (Sunshine Stars)
Mudather El Tahir (Al-Hilal )
Youssef Msakni (Espérance)
3 Mohamed Seguer (ASO Chlef)
Jacques Haman (Coton Sport)
Oumar Kida (Stade
Malien)
Muandro (Muculmana)
Stelio Telinho (Muculmana)
Ifeanyi Egwim (Dolphins)
Edward Sadomba (Al-Hilal)
Kelechi Osunwa (Al-Merreikh)
Lasaad Jaziri (Etoile du Sahel)
Felix Nyaende (Power Dynamos)
Takesure Chinyama (Dynamos-Zimbabwe)
إرسال تعليق