UONGOZI wa timu ya soka ya Yanga umeisogeza mbele sherehe za
kuwapongeza wachezaji wake kwa kufanya vizuri katika michuano ya Kagame
iliyomalizi hivi karibuni.
Yanga katika michuano hiyo iliyokuwa ikitimua vumbi hapa nchini na kushirikisha klabu mbalimbali kutoka nchini wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ilibuka bingwa kwa mara nyingine tena wa mashindano hayo baada ya kufanya hivyo pia mwaka jana.
Akizungumza na Mwananchi jana Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa alisema kuwa wameamua kuzisogeza mbele sherehe hizo kutokana na watu wengi wanao husika na tukio hilo kuwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
"Baada ya kumalizika kwa mfungo wa ramadhani ndiyo tutafanya sherehe hizo ili watu wote kwa pamoja waweze kushiriki na kusherekea kwa pamoja ubingwa Kagame ambao ni wa kwanza kwetu kwa mwaka huu."
Wakati huo huo, mshambuliaji wa Yanga, Mganda, Hamis Kiiza amechaguliwa kuwa mwanamichezo bora wa mwezi Julai wa Shirikisho la Soka Uganda (Fufa).
Uteuzi wa Kiiza umetokana na kufanya vyema katika Michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni huku klabu yake ya Yanga ikijinyakulia kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo.
Kiiza aliwashinda wenzake wawili, Julius Ogwang anaecheza timu ya vijana chini ya miaka 20 na mchezaji wa mpira wa kikapu, Lelis Okan.
Kwa mujibu wa mtandao wa Fufa, Kiiza amekuwa mchezaji mwenye mafanikio makubwa katika klabu yake ya Yanga sambamba na timu yake ya taifa, Uganda Cranes

Chanzo:- Mwananchi
إرسال تعليق