SIMBA SC WAACHA MILIONI NA KITU KWA YATIMA WA MAUNGA

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba SC leo wamehitimisha Wiki ya Simba na Jamii, kwa kutoa misaada yenye jumla ya thamani ya Sh. Milioni 1.5 katika kituo cha kulelea watoto yatima, Maunga Orphanage Center, kilichopo Kinondoni Hananasif, Dar es Salaam.
Baadhi ya wachezaji wa Simba, Emanuel Okwi, Juma Nyosso, Uhuru Suleiman, Meneja Nico Nyagawa, Daktari Cossmas Kapinga, Ofisa Habari, Ezekiel Kamwaga, Katibu Evodius Mtawala na Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ walijumuika na watoto wa kituo hicho kuwafariji.
Akizungumza baada ya kukabidhi fedha taslimu Sh. 500,000 mbali na unga, mchele, sabuni na bidhaa nyingine, Kaburu alisema kwamba huo ni mwanzo tu na watakuwa wakiendelea kusaidia kituo hicho.
“Simba SC ni taasisi kubwa, tunasema tumeguswa na kilio chenu, nasi tunaahidi kuendelea kusaidia kadiri ambavyo tutakuwa tukipokea maombi kutoka kwenu,”alisema Kaburu.
Akitoa shukrani baada ya kupokea misaada hiyo, Katibu wa kituo hicho, Rashid Mpinda aliwashukuru Simba SC na kuwatakia kila heri katika msimu ujao, kuanzia kwenye Ligi Kuu na michuano ya Afrika.
Maunga Orphanage Center kilianzishwa mwaka, 

Post a Comment

Previous Post Next Post